Ijumaa, Februari 09, 2018
Februari 09, 2018, Ijumaa
JUMA LA 5 LA MWAKA
1Fal 11:29-32;12:19
Zab 81:9-14
Mk 7: 31-37.
EPHATHA, FUNGUKA!
“Funguka!” haya ni maneno mazito katika kitendo cha kuamuru. Yapo wazi na ni ya mwisho. “Funguka” sio swali wala sio mwaliko, ni amri. Neno hili lina dhihirisha kwamba Yesu ameamua sasa kutenda. Linaeleza kwamba hana wasi wasi katika kuamua kwake na kutenda. Ameamua sasa kutimiza na anongea mapenzi yake. Na kwa kitendo hiki, kwa upande wake, ndicho kinacho onesha tofauti. Neno hili anavyo liongea linaonesha kwamba Mungu hana wasi wasi anavyo ongea. Kama yeye anaiongoza dunia (kusikia kwa kawaida), ni wazi na dhahiri kwamba anaongoza pia ulimwengu wa kiroho. Anauwezo wakufanya yote yawe mazuri.
Huyu kiziwi hakuweza kuomba msaada, kwasababu hakusikia neno la kuongea. Hakuna aliye elewa alichosema. Lakini watu wenye huruma walimuonea huruma wakamleta kwa Yesu.Yesu anamchukua pembeni kutoka kwenye umati, na anamgusa kwa kidole chake machoni, masikioni na kwenye ulimi, na anasema “efata” (funguka) na masikio yake yanafunguka, ulimi na macho pia. Yesu alitaka kumuonesha huyu kiziwi jinsi alivyomjali na furaha ya huyu aliyeponywa inapaswa imfanye aweze kutenda mema na kuepuka kufanya mabaya kwa masikio yake na ulimi wake. Kwa namna ya pekee, huyu mtu anapaswa kufungua masikio yake kusikiliza neno la Mungu, na kutumia ulimi wake kutangaza huruma ya Bwana.
Tutafakari juu ya neno hilo la Yesu. Tunaomba mamlaka haya matakatifu na ya Kimungu ya Yesu yaongoze maisha yetu. Tunamuomba yeye atuamuru sisi. Tuweze ‘funguka’ leo. Ili tuweze kutumia masikio yetu kusikiliza neno lake na kutumia ulimi wetu kutangaza neno na kuimba sifa zake, kuwa na adabu ya macho pia, kutazama mambo mema na kuacha kutazama yanayo haribu moyo.
Sala:
Bwana, ninakuamini wewe na nina amini unaweza kufanya mambo yote. Ninatambua unapenda kuwa na mamlaka kamili ya maisha yangu. Nisaidie niweze kurudisha maisha yangu kwako na kukuamini wewe unayetosha kuongoza na kuelekeza kila kitendo cha maisha yangu. Yesu, nakuamini wewe kabisa.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni