Alhamisi. 28 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatano, Januari 24, 2018

JANUARI 24, 2018


JUMA LA 3 LA MWAKA WA KANISA


Kumbukumbu ya Mt. Fransisko wa Sales, Askofu na Mwalimu wa Kanisa


2 Sam 2:4-17

Zab 89:3-4.26-29,

Mk 4:1-20


MBEGU NI NENO LA MUNGU

“lakini waliopanda katika udongo mzuri ni wale waliosikia neno la Mungu na kulikubali na kuliacha lizae matunda”.

Katika Injili ya Marko ambayo ni fupi kati ya Injili nne, huwa inatazama kazi za Yesu zaidi kuliko mahubiri yake, tunapaswa kuchukulia kwa makini mafundisho ambayo anayachukua Marko katika Injili yake. Tunaweza kuchukulia mifano aliochagua Marko kama iliyo ya muhimu kabisa. 


Injili ya leo ina sehemu tatu muhimu. Sehemu ya kwanza naya mwisho inaelezea Yesu akitoa mfano na kuuelezea. Katikati Yesu anaelezea kwanini yeye anahubiri kwa mifano. Karibia sura nne za injili ya Marko zimebeba mifano, na Injili ya leo ya Marko imebeba mistari 20 ya sura ya nne. Hivyo mfano wa leo ni wa muhimu kweli kweli. 


Mpanzi ni Mungu Baba. Anayesia neno lake kwa kila mtu, hata kule kuko onekana kuwa kama ujinga kwasababu ya kusia mbegu zake hata katika mioyo migumu ya watu, hiki ni kipimo cha upendo wake kwa kila mtu. Anawapatia watu wake neno hata wale walio na mioyo migumu kama mwamba au jiwe, hata wale waliosongwa na ulimwengu, hata wale ambao machoni mwa mwanadamu hawafai. Changamoto hapa ni kwamba tunapaswa kulima na kutifua udongo wa mioyo yetu ili neno la Mungu liote na kuweka mizizi. Na pia tunapaswa kulipalilia linapo anza kukuwa kwa kufweka miiba (malimwengu yanayo tusonga), ili neno liweze kuzaa matunda mema na kuwafikia wote. 


Neno hili likizaa matunda watu watachuma matunda ya neema na kumshukuru Mungu kwa ajili ya zawadi ya mazao ya neno lake. Mmoja akilipokea neno la Mungu akampenda Mungu na jirani, hata jirani watampa Mungu shukrani kwasababu ya neno lililo ingia ndani ya nafsi ya huyo mtu kiasi cha kuzaa matunda yakawafikia wengine. 


Sala: 

Ee Mungu ninakuomba Neno la Mwanao lizame ndani ya moyo wangu lizae matunda ya upendo, Amani, furaha na utulivu wa kuungana nawe na pia niweze kuwaleta wengine kwako kutokana na matunda yake. Yesu nakutumaini .

Amina

Maoni


Ingia utoe maoni