Jumanne, Januari 16, 2018
Januari 16, 2018
JUMANNE, JUMA LA 2 LA MWAKA
1Sam. 16:1-13
Zab. 89:19-21, 26-27 (K) 20
Mk 2: 23-28
YESU NA SABATO!
Leo Yesu na wanafunzi wake pamoja na Mafarisayo wachache walikuwa wakitembea siku ya Sabato. Wafuasi lazima watakuwa walivutiwa sana na kushikwa na mafundisho ya Yesu, kiasi kwamba walisahau kuhusu sheria ya kufunga na kushika sabato na wakawa wakivunja masuke ya ngano ili kupunguza njaa yao. Waliendelea kufurahia uwepo wa Yesu, bila hatia yoyote. Lakini Mafarisayo wapo makini juu ya kosa la kuvunja sheria ya kufunga na ya Sabato. Sisi nasi tunaweza kuwa watu wakuangalia sheria zaidi bila kuweka upendo ndani ya sheria hizo! Sheria isiokuwa na upendo haijengi utu wa mwanadamu.
Maneno ya Yesu kuhusu hili yananyoosha maelezo moja kwa moja kwamba “Sabato ni kwa ajili ya Mwanadamu, sio Mwanadamu kwa ajili ya Sabato”. Kwa maneno mengine ukweli wote kuhusu siku ya Sababto haikuwa kwasababu ya kutuwekea mizigo mizito, bali, ilikuwa kutuweka huru kupumzika na kuabudu kwa uhuru. Sabato ni zawadi ya Mungu kwetu. Jumapili ni Sabato mpya na ni siku ya kupumzika na kumwabudu Mungu, ni mwaliko wa maisha ya neema.
Tutafakari leo jinsi tunavyo adhimisha siku ya Bwana. Je, tunaona wito wa kuabudu na kupumzika kama mwaliko kutoka kwa Mungu ili kufanywa wapya na kufurahishwa na neema zake? Au unaona kama ni jukumu tu na lazima litimizwe? Mtazamo mpya wa siku hii utaleta maana mpya katika maisha yetu.
Sala:
Bwana, ninakushukuru kwa kuanzisha Sabato mpya kama siku ya kupumzika na kukuabudu. Nisaidie kuishi kila jumapili na siku takatifu zinipasazo katika hali ambayo unapenda wewe. Nisaidie kuziona siku hizi kama zawadi kutoka kwako, ili niabudu na kufanywa mpya. Yesu, nakuamini wewe.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni