Alhamisi. 19 Septemba. 2024

Tafakari

Jumatano, Agosti 24, 2016

Jumatano, Agosti 24, 2016,
Juma la 21 la mwaka

Sikukuu ya Mt. Bartolomayo, Mtume

Ufu 21: 9-14;
Zab 144: 10-13, 17-18;
Yn 1: 45-51


NJOO NA UONE: KUKUTANA NA YESU!

Leo kanisa linafurahia kwa kuadhimisha sikukuu ya Mt. Bartolomayo Mtume. Anajulikana pia kwa jina la Nathanael na alikuwa mmoja wao wa mitume kumi na mbili wa Bwana wetu Yesu Kristo. Alikuwa ni mmisionari akiwa na Philipo na Tomas. Inasemakana alihubiri Injili katika maeneo haya ya, Armenia, India, Persia na Phrygia.

Katika Injili ya leo tunamuona jinsi Philipo anampeleka Nathanaeli kwa Yesu ili aweze naye kukutana na Masiha. Kwahiyo Philipo anatoa ushuhuda ghani kwa Nathanaeli? Badala ya kuchukua muda wakubishana na rafiki yake, Philipo anaamua kuchukua uamuzi wa hekima wa “Kumpele na kumuona” Yesu kwa macho yake mwenyewe, Yesu huyu anayezungumzwa na watu. Philipo alitambua kwamba kukutana na Yesu mtu binafsi inaweza ikabadilisha maisha ya mtu kabisa. Wakati watu wanapopokea neno la Kristo, na wanapoona upendo wake katika matendo, Yesu mwenyewe, kwa njia ya Roho Mtakatifu, anagusa mioyo yao na kufungua mioyo na akili zao kwenye ufunuo wa Mungu.

Wakati Philipo alivyomleta Nathanaeli kwa Yesu, Yesu alifanya kitu ambacho ni Mungu mwenyewe tu anaweza kufanya! Alifungua moyo wa Nathanaeli na mawazo yake ya ndani ukaweza kutamani ufunuo wa Mungu. Nathanaeli aliyatambua maandiko, alisoma Torati na Manabii na alikuwa akitazamia ahadi ya Mungu itimizwe kwaajili ya watu wa Israeli. Nathanaeli alikuwa ni mtu anayemtafuta Mungu kutoka moyoni. Hakufikiri tu kukua katika akili ya elimu ya Mungu bali alifikiri kuhusu jinsi ya kuungana na Mungu pia. Ndio maana alikuwa tayari kukutana na Yesu, na kuona kama huyu mtu anayefanya miujiza kutoka Galilaya kuwa anaweza kuwa Masiha anayesubiriwa.

Mungu ameweka katika kila moyo wa Mwanadamu hamu na tamaa ya kumtafuta, yeye aliyetuumba wote kwa upendo wake. Sisi pia tunaalikwa tuweze kuwa na uhusiano mzuri na Yesu binafsi. Pia tujitahidi kuwaelekeza wengine waweze kukutana na Yesu. Tusiwe chanzo cha kuwapeleka wenzetu kwenye uovu unaowaweka mbali na Yesu. Tuwafariji wale waliokata tamaa, tuwapeleke kwa Yesu kwenye matumaini ya kweli, tuwapeleke wakakutane na Mungu ili aweze kugusa maisha yao. Sisi wenyewe tuimarishe uhusiano wetu na Mungu ili kwa uthabiti wetu tuweze kuwavuta wengine kwa Yesu. Tujaribu kuwa na Yesu daima katika maisha yetu ya kila siku na tuwe mashaidi wake wa kweli.

Sala: Bwana Yesu, jifunue mwenyewe ndani yangu ili niweze kuwa nawe daima katika maisha yangu. Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni