Alhamisi. 28 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatatu, Disemba 18, 2017

Desemba 18, 2017. 

------------------------------------------------

JUMATATU, JUMA LA 3 MAJILIO

Somo la 1: Yer 23: 5-8 Yeremia anatabiri kwamba Bwana “atachipusha shina lenye haki kwa Daudi; kama Mfalme atatawala kwa hekima.”.


Wimbo wa katikati Zab 72: 1-2, 12-13, 18-19 katika siku zake itachanua na haki mpaka mwezi ukome. Atakuwa na huruma kwa wanyonge na kuwaokoa maskini. 


Injili: Mt 1: 18-24 Malaika wa Mungu alimtokea Yosefu katika ndoto na kumwambia kwamba, Mimba aliyo nayo Maria ni kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Na kwamba ataitwa “Emanuel, yaani Mungu pamoja nasi” 

------------------------------------------------

MUNGU ANANYOOSHA MISTARI ILIYOPINDISHWA 

Mungu anapoingia katika maisha ya watu mara ya kwanza husafisha maumivu na kuleta Amani. Haijawahi kusikika kabla ya hapo kwamba mtoto amezaliwa bila kuwa na Baba yake. Maria aliambiwa apokee hali hii isiyo zoeleka inayoenda kinyume na sheria za kawaida. Inahitajika imani na kumwamini Mungu kweli kweli. Pili, Maria alikuwa hajaolewa. Mimba nje ya ndoa kipindi hicho haikuvumiliwa. Angeweza kukataliwa na Yosefu au na familia yake wasinge elewa bila ufunuo wa Mungu. Je, Maria angeongeaje ili watu wamwamini? Yosefu angeweza kukubali na kuamini tu kwamba mtoto huyu ni wa Mungu? Maria pamoja na hayo alimwamini na kumtegemea Mungu na ahadi zake. 


Yosefu, bila shaka jambo hili alilifikisha kwa Mungu katika sala. Hakuwa mwepesi wa kufoka na kukasirika. Mungu alimtunuku sio tuu kwa kumuongoza na kumfariji, bali kwa uhakika kutoka kwake kwamba yeye amemchagua kuwa baba Mlishi wa Mwanae na jukumu hilo lilihitaji Imani kubwa, kujiamini na kumwamini Mungu mwenyezi. 


Tunapoona pango la mtoto Yesu, tunapo ona malaika akininginia, mama mpendwa Maria na Yosefu Jasiri, wachungaji wanaosujudu na mwanakondoo mpolee, mambo yote yanaonekana vizuri kweli. Lakini fikiria; mimba nje ya ndoa, hofu za kuachwa au kutupiwa mawe, aibu ya watu wa njee juu ya wapendwa, na hali ngumu ya kuweza kuelezea hali yenyewe masikioni mwa watu. Ujio wa Yesu ulihitaji kujitoa kweli na kulileta ugumu. Kwetu pia kujikabidhi kwetu kwa Yesu kunaleta ugumu na uchungu wakati mwingine. Kama Maria tunapaswa kumtegemea Mungu, hata pale tunapokumbana na hali za kushangaza na hata kile kinacho onekana hakiwezekani. 


Sala: 

Bwana, sisi tunayafahamu mapenzi yako kwa kila siku inayotokea. Jina lako ni Emanueli, maana yake Mungu yupo pamoja nasi. Tunakuomba ssi tuweze kuwa na uhakika wa ujio wako na kutupatia Imani ya kushikilia ahadi zako. Yesu nakuamini wewe. 

Amina

Maoni


Ingia utoe maoni