Alhamisi. 28 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatatu, Disemba 11, 2017

Desemba 11, 2017. 

Jumatatu, JUMA LA 2 LA MAJILIO

Somo la 1: Isa 35:1-10 Isaya anatoa picha ya “nyakati za Masiha” ni katika uzuri wa jangwa linalo furahi na ubinadamu ulioponywa kutoka katika magonywa yote. 

Wimbo wa katikati: Zab 85: 9-14 tazama, Mungu anakuja kutukomboa. Haki itamtangulia yeye….na Amani itafuata hatua zake.

Injili: Lk 5: 17-26 Sisi tunafanywa hai kiroho na kimwili kama yule aliyepooza. Yesu anathibitisha kwamba anauwezo wakusamehe dhambi kwa njia ya muujiza wa kuponya. 

------------------------------------------------


TAMAA YA KUTAKA KUPONYWA NA KUSAMEHEWA 

Uhakika wa kustahili kwetu katika maisha ni moja ya matunda ya kusheherekea Noeli. Mungu wetu anakuja kutukomboa! Lakini uhakika tulio nao ni kwamba yeye anatusamehe dhambi zetu na kutufanya watakatifu. Na Yesu katika Injili anathibitisha uhakika huo. Tunaona uponya unafanyika katika hali ya Imani kubwa kwa Yesu Kristo. Huyu aliyepooza alikuwa hajiwezi na hivyo ananyanyuliwa juu na kupitishwa juu ya paa mpaka alipo Yesu. Huyu mgonjwa pamoja na hawa marafiki zake walikutana na magumu kabla hawajapata msaada wa Yesu. Kulikuwa na hali ya kukatisha tamaa walipofika katika nyumba ile, lakini hawakukata tamaa. Wanapanda juu ya paa, na kuondoa paa na kumshusha alipokuwa Yesu. Injili inaeleza wazi kwamba ‘Yesu baada ya kuona Imani yao’. Huyu mgonjwa hakumtafuta Yesu mwenyewe, Imani yake kwa Bwana ilisaidiwa na imani ya wenzake. Umoja wao ulifanikisha. Yesu anamponya huyu mgonjwa na anamsamehe dhambi zake. Hapokei uponyaji tu wa mwili bali uponyaji mkamilifu wa kuondolewa dhambi zake zote. 


Tutafakari leo juu ya hamu yetu ya kupokea Msamaha wa Mungu katika maisha yetu. Je, unatamani kupokea huruma ya Yesu na msamaha wake katika maisha yako? Sababu ya Yesu kuja ulimwenguni kutoka mbinguni ni kutusamehe dhambi zetu na kutupatanisha na Mungu Baba. Miujiza mikubwa sio kigezo, kigezo ni msahama. Utakapo pokea zawadi hii ya huruma na msamaha, utamtukuza pia Mungu kwa furaha. Tunaomba kipindi hiki cha majilio kilete furaha mpya katika maisha yetu kwa msamaha wa Mungu. 


Sala:

Bwana njoo, na utuletee sisi Amani. Tutafurahi tukiwa na wewe na kukutumikia kwa mioyo yetu yote. Ninaomba niweze kufurahia katika uwepo wako wa kukutumika kwa moyo wote. Yesu nakuamini wewe.

Amina. 

Maoni


Ingia utoe maoni