Alhamisi. 28 Novemba. 2024

Tafakari

Jumanne, Disemba 05, 2017

Desemba 5, 2017. 

Jumanne, Juma la 1 la Majilio


Somo la 1: Is 11:1-10 Upendo wa juu kabisa wa Mungu wa Masiha utakuja kujulikana. Mfalme atakaye kuja atakuwa anatoka katika shina la Yese, Baba wa Daudi, ambaye Roho wa Mungu atakuja ndani yake. 


Wimbo wa katikati: Zab 71:1-2,7-8,12-13,17 unadhihirisha unabii huu “haki na Amani zitatawala wakati wake na wingi wa Amani milele.” 


Injili: Lk 10:21-24 Yesu anasema kwamba kwa njia ya unabii maneno yake na matendo anatimiza unabii: “Yamebarikiwa macho ya wale wanao ona mnacho ona” 


KAMA WATOTO KATIKA UFUASI

Injili ya leo inaanza kwa Yesu kufurahi katika Roho Mtakatifu. Furaha yake ni kwasababu ya neno lake linaweza kueleweka hata kwa wadogo. Wakati mara nyingine kusoma sana na kufahamu sana yaweza kuwa sababu ya kuikataa Injili, kwasababu hali ambayo inajengwa na elimu ya juu ni ile hali ya kujiona kwamba “unafahamu kila kitu” na hivyo kuwapeleka mbali na Injili. Mungu Baba wa ukweli wote hawezi kudanganywa kwa kitu chochote njee yake mwenyewe, wala hata kwa akili ya binadamu ambayo yeye mwenyewe ameiumba. Hatuwezi kuelewa mafumbo ya Mungu lakini tunaweza kushiriki katika maisha yake. Yesu anashauri kwamba hali ya kuwa kama mtoto ni rahisi sana kupata mafumbo ya Mungu. Akili ya watoto inajazwa na mshangao. Ni rahisi kushangaa makuu yanatotokea ulimwenguni. Watoto wanaweza kuijiingiza vizuri zaidi katika kuyapokea mafumbo ya Mungu kuliko watu wakubwa. Yesu anashauri walio wakubwa kufungua mioyo kwa kumwamini Mungu, ambayo ni uaminifu katika udogo. Na hivyo tutaweza kushiriki katika heri ya Injili ya leo: “Heri macho yanayo ona mnayo ona ninyi” 


Somo la kwanza linatufunulia sisi kuhusu ujio wa Masiha ambaye amejazwa na Roho Mtakatifu na ambaye atakuwa kiongozi mkuu na mfalme juu mbinguni na duniani. Kristo ameshakamilisha utume wake, lakini sisi tunao kuja tunapaswa kupokea ukombozi ulioletwa naye. Nabii katika somo la kwanza anatangaza kipindi kipya ambacho kitaanzishwa na Masiha. Na hivyo amekuja mfalme aliyetarajiwa naye ni Yesu. 


Je, watoto ni akina nani? Ni wale sabini walio rudi kutoka katika utume., watu wa akawaida wasio na elimu kubwa, lakini walio msadiki Mungu. Kwahiyo kama tunataka kuelewa vitu vya Ufalme wa Mungu, tunapaswa kuwa wafuasi, wadogo kabisa! Udogo unamaanisha matendo ya Ufalme katika mambo yetu ya kawaida ya maisha. Wafuasi walihisi zawadi hii ya Mungu walio liita jina la Yesu katika mahubiri yao na kuponya. Leo, Yesu anatuita katika uhusiano naye wa karibu na Pia na Baba yake. Anatuita ‘Rafiki”, sio watumwa” kwasababu ametueleza yote kuhusu yeye; na anatuambia tumuite Mungu “Baba yetu” kama yeye alivyokuwa akimwita. 


Sala: 

Bwana, nipe moyo wa udogo na mnyenyekevu na imani kama ya mtoto. Nisaidie niweze kukuona wewe kama ulivyo, na kuruhusu uwepo wako duniani uingie katika maisha yangu. Yesu, nakuamini. 

Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni