Jumatatu, Agosti 22, 2016
Jumatatu, Agosti 22, 2016,
Juma la 21 la Mwaka C wa Kanisa
Kumbukumbu ya Bikira Maria Malkia
2 Thes 1: 1-5, 11-12;
Ps 95: 1-5;
Mt 23: 13-22.
MALKIA WA MBINGU FURAHI, ALLELUIA!
Baba Mtakatifu Pius XII katika waraka wake “Ad Caeli Reginam” alipendekeza kuwe na desturi na fundisho juu ya Umalkia wa Bikira Maria na alianzisha sikukuu hiyo katika Kanisa. Lakini Umalkia wa Mama una msingi kutoka katika maandiko Matakatifu. Alivyopashwa habari na malaika, Gabriel alitangaza kwamba mwana wake atapokea kiti cha enzi cha Daudi na atatawala milele. Maria alivyomtembelea Elizabeth, Elizabeth alimwita Maria “Mama wa Bwana wangu” katika mafumbo yote ya maisha ya Maria, Maria anahusianishwa na Yesu. Umalkia wake ni ushiriki wake katika ufalme wa Kristo. Tunaweza kukumbuka pia katika Agano la Kale, Mama wa Mfalme alikuwa na nguvu sana katika mahakama.
“Malkia yupo tayari kila wakati kumuomba Mfalme aliyemzaa” alisema Baba Mtakatifu Sixtus IV. Katika Karne ya nne, Mt. Efrem alimuita Maria kuwa ni “Malkia”. Baadae Mababa wa Kanisa na Walimu wa Kanisa wakawa wanatumia jina hilo. Utenzi wa karne ya 11 mpaka karne ya 13 unamuelezea Maria kama Malkia. Rozari ya Kidominiko na Wafransisko katika sala mbali mbali na litania wanamvika Maria taji kama Malkia. Sikukuu hii katika hali ya kufikirika inafuata baada ya sherehe ya Bikira Maria kupalizwa Mbinguni na ndio maana inaadhimishwa katika siku ya oktava ya sherehe hiyo.
Mungu anamimina neema zake kwao wote wanao muamini na anaonesha upendo wake kwa walio wadogo, wanyenyekevu na wote wanaopokea neno lake. Swali la Mama Maria “Itawezekanaje?” hakuuliza kwasababu alikuwa haamini au kwamba alikuwa na wasi wasi bali ni kwamshangao. Yeye ni mtekelezaji wa kweli wa neno la Mungu, aliyetayari kufanya mapenzi ya Mungu, hata inapo onekana kugharimu. Mungu anatupa neema na anategemea sisi tuweze kupokea kwa mapenzi hayo hayo, kwa utii, kwa moyo wote kama Maria alivyofanya. Wakati Mungu anaamuru, anatupa pia msaada wake, nguvu, na njia ya kupokea. Tunachohitaji ni “mapenzi mema” tuzame katika neema zake kwakusema “ndio” ya kweli kwa mapenzi yake na mipango yake juu ya maisha yetu. Tuache neno lake lichukue mwili katika maisha yetu.
Sala: Maria, mtumishi na Mama wa Muumba, Malkia wa Ulimwengu, utombee sisi kwa Mwanao. Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni