Jumapili, Agosti 21, 2016
Jumapili, Agosti 21, 2016.
Dominika ya 21 ya Mwaka C wa Kanisa
Is 66: 18-21;
Zab 116: 1-2;
Ebr 12: 5-7, 11-13;
Lk 13: 22-30.
FANYA HARAKA! KUINGIA MLANGO MWEMBAMBA!
Katika maneno ya ufunguzi ya Injili ya leo, tunamuona Yesu akielekea Yerusalemu. Kitendo cha Yesu kutembea kueleke Yerusalemu (kilele cha safari yake duniani) ni mfano kwetu unaonesha kutembea kwetu kuelekea Yerusalemu mpya (kwa Yesu na kilele cha safari yetu mbinguni). Yesu katika utume wake katika miji na vijiji inatuonesha hamu yake yakutuandaa ili tuweze kuingia Mbinguni, ambao ndio mlango mwembamba.
Yesu leo anatuita kwa haraka zaidi tufanye bidii kuingia katika mlango mwembamba kabla haujafungwa. Tunajiuliza katika akili zetu kwanini kuingia kupitia mlango mwembamba inahusianishwa na kuingia katika Ufalme wa Mungu? Kuingilia kupitia mlango mwembamba katika baadhi ya nyumba zetu, katika Treni, mabasi, pengine katika hali ya haraka au wakati wa shughuli zetu ni jambo la kawaida katika maisha. Tukiwa hatujabeba mizigo au tukiwa na vitu vichache huwa tunapita katika milango hii kwa urahisi zaidi. Pia inakuwa vigumu kuingia kupitia milango hii tukiwa tumebeba mizigo mikubwa, wakati mwingine tukiwa tumebeba mizigo kwa mikono yetu miwili. Sisi pia katika safari yetu ya kiroho, dhambi zetu zote, yote tulionayo (mali katika ubinafsi) vinakuwa vikwazo kwa mtu anayetaka kuingia katika ufalme wa Mungu.
Ilikuwa ni Imani ya Wayahudi kwamba nikwawale tu walio tahiriwa na kushika sheria ya Musa wataokolewa. Wapagani walichukuliwa kama watu wasiofaa na wasiohitaji ukombozi. Swali liloulizwa na huyu mtu kwamba., “ni wachache tu watakombolewa?” linadhihirisha hilo. Yesu leo anabadili mtazamo huo kwa kutoa lugha hii ya picha ya kuingia kupitia “mlango mwembamba”, wote wanaweza kukombolewa kama wataingia kupitia mlano mwembamba.
Sisi Wakristo tunaamini kwamba baada ya kifo tutachukuliwa mbinguni au Yerusalemu mpya. Wengi wetu tunatamani maisha ya starehe na utajiri, nguvu, heshima nk. Na matokeo yake, tunabebesha roho zetu mizigo isiyo yalazima tukijazia chuki, wivu, na mengine. Sasa ni kwajinsi ghani roho kama hiyo iliojazwa mambo mengi namna hiyo inaweza kupita kupitia mlango mwembamba? Ni wazi kwamba mizigo yetu inapaswa ipunguzwe, kifurushi chetu kinapaswa kikungutwe kisafishike ili tuweze kuingia kupitia mlango mwembamba. Yesu anatoa angalisho kwamba kukunguta huku na kusafisha kabisa kunapaswa kufanyike haraka. Hapa Yesu anataka kutuambia kwamba tupo hapa duniani kwa muda mfupi tuu, tena mfupi Sanaa na hatujui tutakufa lini.
Kuwa mfuasi wa Kristo kama Mkristo mbatizwa, tunaweza kufikiri kwamba tutakuwa wakwanza kuingia Mbinguni na kushiriki katika Ufalme wa Mungu. Lakini katika maneno ya mwisho katika Injili ya leo, Yesu anatuambia huo sio mtizamo sahihi. Tusipoweza kuingia kwakupitia mlango mwembamba tutabaki njee ya Ufalme na mbaya zaidi tutabaki njee huku mlango ukiwa umefungwa milele. Tuisikie sauti hii ya Yesu sasa na tufanye haraka, tukijua kwamba ametupa wito huo kwasababu anataka sisi wote tushiriki naye katika Ufalme wake.
Sala: Bwana, naomba niishi kuendana na Injili yako, naomba niwe na roho ya unyenyekevu ili niweze kushiriki katika Ufalme wako. Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni