Alhamisi. 28 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatano, Novemba 22, 2017

Jumatano, Novemba 22, 2017. 

Juma la 33 la Mwaka

Kumbukumbu ya Mt. Sesilia, Bikira na Shahidi

2 Mak 7: 1, 20-31;

Zab 17: 1, 5-6, 8, 15 (K) 15;

Lk 19: 11-28.


KUWA WAZALISHAJI KWA AJILI YA UFALME WA MUNGU! 

Katika Mfano wa Injili, wakati Mfalme alivyorudi alihitaji hesabu ya kila mmoja. Sehemu hii inamalizia kwa kusema “kila mmoja aliye na vingi ataongezewa, na asiyenacho hata kile kidogo kitachukuliwa. Lakini kwa hao maadui wangu ambao hawakupenda mimi niwe mfalme wao, walete hapa na kuwangamiza mbele yangu”. Yesu yupo mkali kweli kwa hao wanaoenda kinyume na mapenzi ya Mungu. 


Watumishi watatu walikuwa wamepewa talanta. Mmoja alitumia vizuri akapata zaidi, wa pili alitumia akapata zaidi, lakini watatu hakufanya kitu. Ni huyu mtumishi ambaye hakufanya kitu ndiye anaye lengwa. Tumekuwa tukiongea mara nyingi kuhusu huruma na ukarimu wa Yesu na tupo sawa kuongea hivyo. Yeye ni mwenye huruma na mkarimu kupita yote. Lakini pia ni Mungu wa haki kweli. Katika mfano huu tuna makundi mawili ya watu wanaopokea haki ya Kimungu.


Kwanza kabisa tuna wale Wakristo ambao wanashindwa kuhubiri Injili na kushindwa kutumia kile walichopewa. Wanakaa tu kimya na Imani yao, na mwishowe wanaishia kupoteza hata Imani kidogo walio nayo. Pili, kuna wale ambao wanapinga Ufalme wa Yesu na ujengaji wa utawala wake hapa duniani. Hawa ni wale wanahusika katika kujenga utawala wa shetani katika hali mbali mbali. Matokeo ya maovu yao ni maangamizi yao wenyewe. 

Katika somo la kwanza tunaona uaminifu wa mama na watoto wake licha ya kutishiwa kuuwawa kwasababu ya kutokula nyama haramu iliowekwa kwa miungu ya mfalme. Walisimama imara katika sheria ya Mungu. Uaminifu huu unahitajika kwa Imani yetu. Tafakari leo juu ya umuhimu wa Injili na kumfuata kwako Yesu. Kama kuna kitu kinapungua, omba neema ya kupewa ujasiri na kuwa shuhuda wa Yesu na ufalme wake. 


Sala: 

Bwana, ninaomba nisichezee neema ulizonipa wewe. Nisaidie daima nizitumie daima kueneza ufalme wako. Nisaidie niweze kuona furaha na neema kwa kufanya hivyo. Yesu, nakuamini wewe. 

Amina

Maoni


Ingia utoe maoni