Alhamisi. 28 Novemba. 2024

Tafakari

Jumanne, Novemba 14, 2017

Jumanne, Novemba 14, 2017, 

Juma la 32 la Mwaka

Hek 2: 23 – 3:9;

Zab 34: 1-2, 15-18 (K) 1; 

Lk 17:7-10.

 

MTUMISHI ASIYE NA FAIDA! 

Mtumishi na huduma zake zinaelezea uwepo wa mfuasi wa Kristo. Ni hivyo hivyo kwa kanisa na watu wake. Utume wa Kanisa ni utume kwa Mungu na mataifa. Kufanya uhusani huu kwa kitu kingine kwa ajili ya faida binafsi ni kufanya wengine kama chombo. Kuna watu wengine wanafanya mambo makubwa kwa jina la dini na Mungu. Kuna matendo ya huruma yanayofanywa na watu wa dini nyingine pia. Lakini mara nyingi wengi hupotea wanapo sahau kwamba chanzo cha utume wote ni Mungu, wakati wanapo pandisha majina yao na kuwa makubwa kuliko jina la Mungu. 


Kila kitu tulicho nacho hata sisi wenyewe ni mali ya Mungu na viumbe vyote ni vyake. Nguvu zetu, muda na yote tulio nayo ni mali ya Mungu na tunapaswa kutumia mali hizi kwa ajili ya utukufu na sifa yake. Kila mafanikio tunayopata sio malipo bali ni neema zake na mwishowe kwa yule mtumishi atakaye kuwa mwaminifu ataambiwa “Vyema mtumwa mwema na mwaminifu ingia katika furaha ya Bwana wako” (Mt 25:21)


Yesu anaonesha wazi kuhusu huduma yetu ya Kikristo kwa wengine, ikiwa ni kwenye familia au katika hali nyingine, lazima tuwe na hali ya huduma. Tunapaswa kuhudumia kwa upendo licha ya kueleweka vibaya au mapokezi mabaya kutoka kwa wengine. Tunapaswa kutumikia na kutimiza majukumu yetu ya Kikristo kwasababu ni kitu kizuri cha kufanya na kwasababu ndicho Mungu anachohitaji kutoka kwetu. Tafakari leo juu ya mwamko wako wa kuwahudumia wengine. Jaribu kuongelea maneno haya ya Injili ndani ya maisha yako. 


Sala:

Bwana, nisaidie niweze kutumikia kwa moyo wote na kwa upendo kwa wengine. Nisaidie niweze kujitoa mwenyewe licha ya mtazamo mbaya wa wengine, niweze kupata furaha kwa kitendo chenyewe cha upendo. Yesu, nakuamini wewe.

Amina.


Maoni


Ingia utoe maoni