Alhamisi. 28 Novemba. 2024

Tafakari

Jumamosi, Novemba 11, 2017

Jumamosi, Novemba 11, 2017. 

Juma la 31 la Mwaka

Kumbukumbu ya Mt. Martini wa Tours

Rom 16:3-9, 16, 22-27;

Zab 144:2-5, 10-11; 

Lk 16: 9-15.

 

KUVUNJIKA KWA UKWELI WA NAFSI ZETU 

Kuja kwa mitandao ya kijamii, huku ikileta mafanikio makubwa, imeleta pia kitu tunachoweza kukiita “HKM” (Hofu ya Kukosa Matukio). Tangu simu za “smartphones” ziingie zimerahisisha mawasiliano katika kazi kila mara. Lakini zimeleta pia “hofu ya kukosa matukio” “HKM”. Hili linawafanya watu kila mara awe anatazama simu yake ili asipitwe, kuangalia ujumbe, facebook, hata wakati mwingine kuchati wakati wakiwa wanakula mlo wa pamoja nyumbani au wakiwa wamehudhuria sherehe ya kuzaliwa ya rafiki nk. Wakati mwingine tunakuwa na hofu juu ya uchaguzi waliochagua watu wengine. Je, kuna mwingine amenunua simu mpya? Ni iphone au ni ipad? Je, rafiki yangu atapa hoteli ya kisasa yenye kuvutia? Je, atapata mtu wakumtengenezea nguo zuri?  Tunajisikia vizuri baada tu ya kusoma ujumbe wa wenzetu kutoka facebook, nakujiuliza kuna tukio limenipita kweli? Hali hii na hamu hii ambayo inawaathiri watu 4 kati ya kumi kila siku, inatuonesha sisi hofu tulio nayo kuhusu wengine, tuna mashaka kweli kwa vitu ambavyo hatuna na tunakosa vile ambavyo tunavyo sisi wenyewe. Sisi pia tunapenda sana vitu vyetu vipokee sifa kwa wengine, na kama hatujapata sifa tunaumia kweli. 


Je, una hofu zaidi ya watu kuhusu maisha yako au hofu ya nini Mungu anawaza juu yako? ‘Mungu anafahamu moyo’ anafahamu sisi ni wanani kutoka ndani. Mara nyingi sisi tunahangaika sana kuhusu hofu yetu juu ya watu wanawaza nini kuhusu mimi. Injili ya leo inaenda ndani katika mioyo ya Mafarisayo, wao walikuwa na hali ya kuogopa sana wanaonekana je machoni pa watu, na kusahau, Mungu anawaonaje mioyoni mwao. Wakati mwingine kama Mafarisayo sisi nasi tunakazana sana kutaka kuonekana vizuri machoni pa watu, wakati huo huo Mungu anafahamu undani wa mioyo yetu na anajua sivyo ilivyo. Wakati mwingine watu wanaweza kuwa na picha tofauti juu yetu, kitu ambacho kinaweza kutufanya sisi pia tuumie. Wakati haya yanatokea tunaweza kushikwa na hasira na kuanza kujisafisha na hata kuwachukia wengine. Lakini katika hili ni kipi kilicho cha muhimu? Sisi tunapaswa kuwa na hofu ya nini? Ukweli ni kwmaba tunapaswa kuwa na hofu ya jinsi Mungu anavyo tuona sio kuogopa yale yasio ya muhimu. Tafakari juu ya hali yako ya kuogopa maneno ya watu kuliko dhambi unazo mtendea Mungu. Tambua Mungu anataka uishi maisha ya kweli ya jinsi unavyo jiweka mbele za watu. Ogopa tu kila ambacho Mungu anajua juu yako, mambo mengine mwachie yeye. Mwisho wa vyote hilo ndilo la muhimu. 


Sala:

Bwana, nisaidie niweze kuona kile ambacho kipo ndani ya moyo wako na niweze kujishughulisha na jinsi unavyo niona mimi. Yesu nakuamini wewe.

Amina

Maoni


Ingia utoe maoni