Alhamisi. 28 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatatu, Novemba 06, 2017

Jumatatu, Novemba 6, 2017.

Juma la 31 la Mwaka

Rom 11:29-36; 

Zab 68:30-31, 33-34, 36-37; 

Lk 14:12-14,


CHUKUA NJIA INAYO PITWA MARA CHACHE! 

Luka leo anaelezea tukio ambalo Yesu amealikwa na Mfarisayo nyumbani kwake kwa cha kula cha jioni. Kipindi cha Yesu ilikuwa ni kawaida kwa watu kukaribisha marafiki, ndugu na jamaa kula. Na hakuna aliye kaa mezani na mtu ambaye hamfahamu. Walikaa tuu mezana na wale watu ambao ni marafiki wao. Lakini Yesu hafurahii hali hii ya tabia. Ana agiza kuvunja mipaka na kuwaalika wale waliotengwa, maskini, viwete na vipofu. Yesu kwa kutualika kwa hili anatualika kwenye aina ya utakatifu. “utabarikiwa kwa sababu hawana namna ya kukulipa” Tunapaswa kutenda bila kuwa na maslahi binafsi ili tuweze kupata Baraka hizi. .Yesu anaialika jamii tena ili iweze kuondoa aina zote za matabaka na mipaka na kuhubiri Injili ya upendo. 


Sisi mara nyingi tunaanguka katika mtego wa kutafuta maslahi, hasa kwa tuzo ambalo ni la mara moja. Lakini Injili inatuleza kwamba maisha yetu tunapaswa kuyaishi kama vile hamna mshahara hapa duniani. Bali tunapaswa kungojea mshara wetu mbinguni. Hili linaweza likawa ngumu kuliishi, kwani halihitaji malipo kutoka kwa mwingine na hivyo kufanya kazi kwa uhuru kwa ajili ya wengine ni utakatifu wa maisha. Kwa kuonesha kujali na huruma kwa watu, tunamuiga Mungu wetu mwenye huruma na kufanana naye. Hii ndio thawabu kubwa zaidi kuliko ile ambayo tungeweza kupata kutoka kwa mwingine. 


Sala:

Bwana, nipe mimi moyo ambao umejaa huruma na Msamaha kwa wote wa hitaji. Ninaomba nijitolee kuwatunza bila ya kutafuta faida binafsi. Ninaomba matendo haya ya huruma viweze kuwa sababu ya kupata utakatifu wangu. Yesu nakuamini wewe.

Amina


Maoni


Ingia utoe maoni