Alhamisi. 28 Novemba. 2024

Tafakari

Jumapili, Novemba 05, 2017

Jumapili, Novemba 5, 2017. 
Dominika ya 31 la Mwaka A wa Kanisa 

Mal 1:4 – 2:2, 8-10; 
Zab 130: 1-3; 
1 Thes 2:7-9, 13; 
Mt 23:1-12


UFARISAYO NDANI MWETU!
Katika somo la Kwanza mwandishi wa kitabu cha Malaki aliishi kipindi cha mwanguko wa dini. Baada ya kurudi utumwani Babuloni Waisraeli walijikita sana katika kujenga hekalu. Lakini kwasababu ya kukutana na matatizo wanakata tamaa. Wanapoteza ujasiri kwa Mungu na kuacha sala na wanajiingiza katika hali ya kuwa wavivu wa sala. Na matokeo yake ni kuanguka kwa maadili. Ufisadi/rushwa ikatawala kila pande. Ukosefu wa haki, talaka kila upande, na wafanyakazi wanadhulumiwa. Kwa kipindi hiki, nabii aliyekuwa amezoeleka alikuwa ni Malaki, ambaye jina lake maana yake ni “malaika wa Mungu” akifanya kazi kuleta neema sehemu isiokuwa na neema. Anawataja kabisa wanaohusika kwanza kabisa ni: makuhani wa hekalu, ambao wanahusika na udhaifu huu. Lawama ya nabii inaanza kwa kuwambia kuhusu kutokuwa waaminifu ya kutenda kazi zao za kidini. Wanamtolea Bwana, wanyama walio wagonjwa, kondoo vilema, wanyama walio ibwa (Mal 1:8-14). Kwa kutoa sadaka mbaya, wanyama viwete, hawa makuhani walikuwa wakitafuta faida binafsi. Walikuwa wakijifanya kuhudumia lakini walikuwa wakitafuta faida kutoka kwa waamini. Na hivyo kuwafanya watu waone Mungu sio wa muhimu na kwamba wanaweza kumfanya nae utani tu wapendavyo. Sehemu ya pili ya somo, makuhani wanalaumiwa kwa jambo kubwa zaidi. Kazi yao ilikuwa kuwaonesha watu njia lakini wao wenyewe hawatembei katika njia hiyo, na kuwafanya watu wanao waamini kukwame. Mungu anaingilia na anaonesha unafiki wao na ana ahidi na kwuwaambia kwamba “nitahakikisha kwamba hakuna hata mmoja atakaye kujali, wala kukuheshimu wewe,”

Katika somo la Injili tunashangazwa na lugha kali ya Yesu. “Ole wenu Mafarisayo na waandishi,Wanafiki”. Hatujazoe Yesu akiongea katika hali ya namna hii. Ni vizuri kuwa makini na jinsi mwandishi alivyo tumia lugha na maneno haya, kama mtu anataka kurejea kwenye maneno haya, sio tu kwa Wayahudi wa kipindi hicho bali pia kwa Wakristo wa leo. Maneno ya Yesu ni makali kwa sababu aliona kukataliwa huku ni hatari kwao. “Yesu hasemi ole tu kwa Waandishi na Mafarisayo wa kipindi chake, alikuwa akiongea na umati na wafuasi wake (Mt 23:1), kwani walikuwa katika hatari ya kuanza kutenda kama Mafarisayo. Sisi nasi tunaitwa kusikiliza maneno haya. 

Farisayo kwanza kabisa alikuwa ni yule ambaye anachukua kiti. Kwa kila sinagogi kulikwa na “kiti cha Musa” ambacho kilikaliwa na Mwandishi ambaye atafafanua maandiko. Maneno ya Rabi ambaye alikuwa amekaa pale, alama ya kwamba Musa ameketi anawafundisha watu sheria ya Mungu. Yesu anatumia ishara ya kiti hichi kuelezea mamlaka. Sheria ambayo ilikuwa ni alama ya uhusiano na Bwana, waliipunguza na kuwa sio sehemu ya kumfuahia Mungu na kukaribishwa naye, hili linaonesha tabia ya kiroho ya Mafarisayo.

Tabia ya pili ya Mafarisayo ni kukosa mpangilio. Fariayo ni yule ambaya nasema fanya alafu hafanyi. Yeye ni mtu wakujitoa, anayeongea maneno mazuri, ya upendo. Amani, anaheshimu wengine, lakini yeye mwenyewe hajiingizi katika kuayatenda. 

Sifa nyingine ya Mafarisayo ni kuweka mizigo mizito juu ya mabaga ya watu wengine. Wanapunguza imani juu ya Mungu, upendo na huruma yake na kuwa kitu cha kidini. Waliweka sheria ngumu, kuosha mikono, kufanya maisha magumu, kusababisha hofu badala ya kuleta Amani ya ndani. Hivyo dini ya Kiyahudi inawakilishwa na mapipa matupu yasiokuwa na divai. Ni sawa na karamu ya harusi isiyokuwa na divai na furaha kwasababu inakosa upendo, uhuru na ujasiri wa kumwelekea Mungu. (Yn 2:1-11). Waandishi walio weka mizigo hii hawakunyoosha hata kidole hata kimoja kuwasaidia watu, waliokandamizwa na uzito wa sheria hizi. 

Sifa nyingine ya Mafarisyo ni kujionesha, kutaka kuonekana. Yesu aliwaita wanafiki kwasababu wanafanya mambo mazuri mbele ya watu, kwenye masinagogi, kando kando ya barabara, kufunga kwa kipindi kirefu na kukucja uso ili watu wawaone.

Katika somo la leo mambo mengine yameelezwa ambayo mafarisayo wanayatumia ili kutambuliwa. Kukaa sehemu za heshima, kukaa sehemu za mbele za heshima ili waonekane na watu, na kuvaa mavazi makubwa wakati wa sala. Mwishoni mwa Injili ya leo inaonesha sura ya jinsi Mkristo wa kweli anapaswa kuwa, ambapo ndani yake kila aina ya utengano na hali kubagua huondolewa. Ni katika jamii na dini kwamba hali ya ukubwa na udogo inaoneakana. 

Katika jumuiya ya Wakristo majina ya heshima yanapaswa kuwa ndugu, kaka wafuasi, watumishi na yote ambayo yanaonesha huduma. Sio kuitwa mabwana, marabii na majina yakuonesha heshima za ulimwengu! Maneno ya mwisho ya Injili yanaonesha ni kitu ghani tunapaswa kufanya ili kukwepa chachu ya ufarisayo. “aliye mdogo kati yenu na awe mtumishi wa wote. Kwani yule anaye taka kuwa mkubwa na ajishushe, na ambaye atajishusha atakwezwa” Unyenyekevu huja kabla ya heshima. (Meth 18:12)

Sala:
Bwana, ninaomba niwe wazi kwa Injili kila inapo hubiriwa. Bwana ninaomba nisikilize neno lako kwa ujasiri zaidi linapo hubiriwa na kuwa imara kukwepa hali ya Kifarisayo. Ninkuomba nikuige wewe pekee, mfano wa Unyenyekevu. Yesu nakuamini wewe.
Amina 

Maoni


Ingia utoe maoni