Jumamosi, Novemba 04, 2017
Jumamosi, Novemba 4, 2017.
Juma la 30 la Mwaka
Kumbukumbu ya Mt. Karoli Boromeo, Askofu.
Rom 11: 1-2, 11-12, 25-29;
Zab 94: 12-15, 17-18 (K) 14;
Lk 14: 1, 7-11.
HATARI YA MAJIVUNO
Kila mwanadamu anatamani kuwa mtu maarufu. Tunakazana kuheshimiwa na kutambuliwa na watu. Lakini jitihada hizi za mtu zinaweza kumuangusha. Katika somo la kwanza la Mtume Paulo kwa Warumi, Paulo anazunguzia juu ya upofu wa mafarisayo na Waandishi, walikuwa wataalamu wa maandiko na sheria lakini kwa sababu ya majivuno yao wakashindwa kumtambua Masiha ambaye Maandiko yamemuongelea. Katika hali zetu za anasa, kutafuta mamlaka, tunakuwa na hali ya kusahau sisi ni akina nani. Viongozi wazuri wanaanza kuwa wadhulumu kwa njia ya kukosa haki. Unyenyekevu kwa njia nyingine ni kutambua sisi ni akina nani. Na unaaza kwa kutambua kuwa Mungu ni chanzo la lengo la maisha. Hivyo nikutumia vipaji vyetu vyote, vile ambavyo vinatutambulisha na Mungu, kumpa yeye utukufu na kuwasaidia ndugu zetu, kaka na dada zetu.
Yesu kwa kutoa mfano wa karumu ya harusi, moja kwa moja aliwaongelea wale waliokuwa naye mizani wakila, katika nyumba ya Farisayo. Bilashaka wale waliokuwa wakimsikiliza waliguswa na hali zao za kujitazama wao wenyewe na kushindwa kuwatazama wengine. Itakuwa ni jambo la aibu na kuaibishwa wakati umekaribishwa viti vya mbele alafu baadae wanakushusha na kukuweka katika sehemu ya mwisho. Aibu hii ni kwa wale waliokamatwa na anasa za ulimwengu. Yesu alitumia mfano huu kwa kuonesha hatari ya kuishi katika hali hiyo ya majivuno. Anaendelea kusema “kwa yeye yule ambaye atajikweza atashushwa, lakini yule ambaye atajishusha atakwezwa”.
Tunapaswa tuchuguze dhamiri zetu kila siku juu ya majivuno. Majivuno yanachukuliwa daima kama “mama wa dhambi zote” kutokana na sababu. Majivuno yanapelekea utendaji wa dhambi nyingine katika namna mbali mbali, ni chanzo cha dhambi nyingine zote. Hivyo kama tunatamani kuwa wakamilifu katika maisha ni vizuri kukimbilia unyenyekevu wa kweli siku zote. Unyenyekevu si kitu kingine zaidi ya kuyaona mambo kama yalivyo. Mtu mnyenyekevu anajiona mwenyewe katika ukweli wa Kimungu. Hili ni ngumu kulifanya kwasababu inatubidi sisi kujiona na kuutazama udhaifu wetu na kwamba Mungu ndiye tegemezi letu. Tunaweza kufanya mambo mengi ulimwenguni kwa kutumia nguvu zetu wenyewe. Lakini hatuwezi kupata furaha ya kweli mpaka tumefungua mioyo yetu katika hali ya kweli na kumtegemea Mungu kwa kila kitu. Unyenyekevu unatusaidia kuosha mioyo yetu kutoka katika kitu kigumu ambacho tumeshindwa kukitoa rohoni mwetu. Tujichunguze leo ni kwa jinsi ghani tulivyo huru kutoka katika majivuno yetu? Tutembee katika njia ya unyenyekevu ndugu yangu.
Sala:
Bwana, nifanye mimi niwe mnyenyekevu. Safisha kabisa majivuno katika maisha yangu ili niweze kukujeukia wewe na wewe pekee. Yesu nakuamini wewe.
Amina
0 Imependwa
0 Maoni
Maoni
Ingia utoe maoni