Alhamisi. 28 Novemba. 2024

Tafakari

Ijumaa, Novemba 03, 2017

Ijumaa, Novemba 3, 2017, 

Juma la 30 la Mwaka

Rom 9: 1-5;

Zab 147: 12-15, 19-20 (K) 12; 

Lk 14: 1-6.


 

KUWA NA HURUMA

Leo Yesu anwauliza Mafarisayo swali “je, ni kinyume cha sheria kumponya mtu siku ya Sabato?” Mafarisayo hawana jibu. Baada ya kumponya mtu aliyekuwa na ukoma, anawaonya Mafarisayo kwa kushindwa kuonesha huruma, na badala yake kutumia sababu za kisheria.

Mafarisayo hawakuwa na huruma kwa ndugu zao, huyu mtu mwenye ukoma, walikuwa wakijishughulisha na Sabato. Yesu anawauliza kwa mfano alikuwa mwana wao au alikuwa ni punda wao? Yesu anaonesha mioyo baridi ya Mafarisayo, ambao walifikiria kwamba punda ni zaidi ya wana wa Mungu waliokuwa wagonjwa na maskini. 

Kama tukijaribu kumwangalia huyu mtu alieponywa. Ugonjwa ambao ulikuwa ukimtesa ulikuwa ni ukoma, ambapo mwili hutoa maji maji. Sisi kama Mafarisayo huenda tukawa tunaugua ugonjwa kama wa Mafarisayo-pengine si katika hali ya mwili. Hili linakuja pale ambao tunajaza mioyo yetu na ubinafsi na kushindwa kupenda kizuri kwa ajili ya wengine. Ni Yesu mwenyewe anayeweza kuondoa ukame wetu na ubinafsi wetu wa kushindwa kuwapenda wengine kwa uhuru.

Cha muhimu ni kuona mwitikio wetu juu ya wale wanao hitaji msaada wetu, huwa tuna visingizio vingi vya kutoa. Kwa mfano swala la wakimbizi, Baba mtakatifu Fransisko la kuwasahauri parokia na wakristo kuwakaribisha wakimbizi halikupokelewa sana. Swala hili wamelichukulia katika mijadala. Lakini mbaya zaidi hakuna hata tendo lolote la huruma wanalopendekeza wale wanao pinga. 

Leo, tujiulize sisi wenyewe kama nasi tuna mioyo baridi. Je, tupo tayari kuvuka mipaka ya akili zetu na mipaka ya roho zetu kwa aili ya kuwa wakarimu? 

Sala:

Bwana Yesu njoo katika moyo wangu, katika hali yangu ya maisha. Njoo zama, katika kazi, kati ya marafiki, katika magumu yangu, wakati wa matatizo, na katika vitu vyangu. Nisaidie mimi niweze kuwa mkarimu kwa ndugu zangu. Yesu, nakuamini wewe.

Amina

Maoni


Ingia utoe maoni