Alhamisi. 28 Novemba. 2024

Tafakari

Ijumaa, Oktoba 27, 2017

Ijumaa, Oktoba 27, 2017
Juma la 29 la Mwaka

Rom 7: 18-25;
Zab 119: 66, 76-77, 93-94 (K) 68;
Lk 12: 54-59.


KUFAFANUA NYAKATI ZETU

Leo katika Injili ya Luka inafafanua ni kwa jinsi gani baadhi ya watu walikuwa na uwezo wakusoma majira kwa mfano mawingu na mvua kipindi cha Yesu, lakini  wakashindwa kufafanua kipindi cha Yesu ambacho Yesu mwenyewe alikiweka mbele ya macho yao kwa kuhubiri Neno la Ufalme wa Mungu.  Je, si kweli kwa nyakati zetu pia?

Sisi tumebobea sana katika teknologia ya sayanzi na tunajivunia sana hali hii. Lakini mara nyingi tunakosa ujumbe ambao Mungu anataka kutuambia.  “alama za nyakati” ulikuwa ni ujumbe muhimu sana wakati wa mkutano wa Vatican II ukituita kufafanua Neno la Mungu kulingana na nyakati zetu  bila kuharibu ujumbe wa Yesu na mtazamo wa kanisa la kwanza na ujumbe wa Mababa wa kanisa. Kufafanua wakati wetu maana yake kujikabidhi wenyewe kwenye ukweli. Tunapaswa kumtafuta Yesu kwa moyo wote na kutaka yale yote ambayo yapo kwa ajili yake na kuacha yale yasio ya kwakweli. 

Jamii yetu inatuwekea maadili mbali mbali, tunaweza kujikuta sisi tukivutwa huku na huku. Tunaweza kukuta kwamba akili zetu zimechukuliwa na tukakuta hata kile muhimu cha ubinadamu wetu kimeharibiwa. Mfano sheria za kutoa mimba, kuwaua watu kwa sindano eti kisa anateseka mno! Ndoa za kijadi!  Maadili yetu yamevamiwa katika kila nyanja. Kusoma alama za nyakati ni kuwa makini na kuyaona yote jinsi ulimwengu unavyo jichanganya kila wakati na kulinda ukweli. Huku tukiona makosa yanayoletwa kwenye maadili na tamaduni zetu. 

Tafakari leo kama upo tayari kumkaribisha Roho wa ukweli akuongoze katika kweli. Kuutafuta ukweli na kubaki nao ndio njia pekee ya kulinda maadili yetu na kukwepa madhara yanaoletwa na teknolojia.

Sala:
Bwana, nisaidie niweze kusoma alama za nyakati na kuona makosa yote yanayo tokana nayo na pia uzuri wako unaoneakana katika hilo. nipe ujasiri na nguvu niweze kukwepa kile kilicho kiovu  na kutafuta kile ambacho kinatoka kwako. Yesu nakuamini wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni