Jumatatu. 13 Mei. 2024

Tafakari

Alhamisi, Agosti 18, 2016

Alhamisi, Agosti 18, 2016,
Juma la 20 la Mwaka

Eze 36:23-28;
Zab 50:12-15, 18-19;
Mt 22:1-14


SHEREHE YA HARUSI!

Inafarijisha sana, kufikiri mbinguni kama sehemu ya sherehe ya harusi/karamuni. Itakuwa Yesu aliipenda sherehe ya harusi na akaona ni kielelezo/mfano mzuri wa kutueleza sisi alicho tuandalia Mungu.

Katika somo la injili, mfalme anashangazwa kwamba ameandaa sherehe kubwa ya harusi ya mtoto wake lakini wageni walioalikwa hawana muda wakuhudhuria karamu hiyo. Kuna mambo mengi katika mfano huu. Kwa hakika cha kwanza ni kuhusu kualikwa. Mungu anatualika na hatulazimishi anatupa uhuru. Tunaweza kukubali au kukataa. Tupo huru. Inavyoonekana alivyotendewa yule asiyevaa vazi la harusi inaweza kushangaza kidogo. Tuliangalie hili kwa ukaribu zaidi. Wakati mfalme anavyomtambua “alikaa kimya!” iko wazi kutoka kwenye somo kwamba huyu mtu hakuwa na vazi la harusi kitendo cha kukosa kuwa makini na heshima kwa mfalme. Si kwamba huyu mgeni alishindwa kuwa na vazi

Sisi tumealikwa kwenye urafiki na Mungu. Tumepewa neema ya utakaso kama zawadi, lakini ni zawadi inayohitaji kujishughulisha. Tunapaswa tuishi ujumbe wa Ukristo unaoweza kutulazimu kubadili mitizamo yetu, tabia na aina ya maisha. Huyu mtu aliyeelezwa kwenye injili hakuwa na lakusema. Hakuwa amejiandaa kuingia katika karamu.

Mfano wa karamu unaoendana sambamba na mfano huu ni Ekaristi Takatifu- zawadi ambayo ni ya hali ya juu kabisa ambayo hatuwezi kujitetea kuwa haki yetu, zawadi tusio stahili. Je, tunamaanisha kweli maneno tunayo sema kabla ya komunyo; Ee Bwana sistahili uingie kwangu lakini sema neno tu na roho yangu itapona? Kwahiyo leo, tunaomba mfano huu, ututikise mioyo yetu nakututoa katika uvivu na hali ya kuridhika na hali yetu. Tusimchukulie Mungu kwa mizaha! Tumpende Mungu kweli tuwe tayari kutoa sadaka yote yanayotufanya tujifariji binafsi na kushindwa kujiweka tayari kwa karamu na hapo kiaminifu tuweze kusema kwa ujasiri “Kufanya mapenzi yako, Ee Mungu, ndio furaha yangu”.

Sala: Ee Mungu, ninakushukuru kwa kunialika kwenye karamu yako ya Mbinguni. Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni