Jumapili, Oktoba 08, 2017
Jumapili, Oktoba 8, 2017.
Dominika ya 27 ya Mwaka wa Kanisa
Isa 5: 1-7;
Zab 79: 9,12-16, 19-20;
Flp 4: 6-9;
Mt 21: 33-43
YESU, MSINGI WA UKOMBOZI WETU!
Akimuongelea Kristo ambaye ndiye jiwe kuu la Msingi ambalo lilikataliwa na waashi, Mathayo anasema “ambaye anaanguka juu ya jiwe hili, atavunjika vipande vipande, na ambaye ataangukiwa na jiwe hili atakuwa mavumbi matupu” (Mt 21:44). Yesu na Injili yake ni “Jiwe”. Ambalo linafunga akili na maarifa ya ulimwengu huu, ujanja, na mambo yote au picha yeyote ile inayojengwa na Mwanadamu kuhusu Mungu. Wakuu wa ulimwengu huu watengenezaji wa mnara mwingine wa “Babeli” wanalikataa jiwe hili kwasababu haliaendani na mambo yao, linafuta ndoto zao na kuharibu falme zao. Wanajaribu kuliondoa lakini Mungu alilichagua liwe sababu ya ukombozi. Yeyote atakaye lifanya kama msingi wa maisha yake hatajutia kabisa.
“Siku za mwisho..mmoja ataweza kukaa chini ya mtini kwa Amani na kwa uhuru au chini ya zabibu na wala hakuna atayemfanya aogope” (Mik 4:1-4). Kwa sura hii nzuri ya kikijini, Mika alielezea Amani na furaha ya kila Mwisraeli aliokuwa akitamani. Zabibu ni ishara ya Amani, umoja wa familia, furaha na sherehe. Wimbo ulio Bora anaota juu ya mtu anaye kimbia katikati yake akiwa na mpendwa wake wakati wa asubuhi tulivu: “twende zetu tukatembee katika zabibu na kuangalia kama zimechipua na kuchanua maua. Na pale nitakupa mapendo yangu” (Wimbo 7:13). Katika hali hii ya utamaduni, ambapo shamba la mzabibu linahusishwa na wito wa mapendo. Furaha ya mkulima huyu ni sawa na furaha ya upendo alionayo kwa yule anaye mpenda mchumba wake. Zabibu hizi zilipandwa katika milima mizuri. Ardhi isiyo na miiba, isiyo na magugu wala mawe yaliyo shambani. Alijitolea kwa kila kitu akitegemea mavuno mazuri. Bali zabibu mitwi zimetokea na hivyo anaumia sana, kama vile moyo wa mtu aliye umizwa katika kuachwa na mchumba wake, upendo unabadilika na kuudhika na kukasirika.
Huyu mkulima anajiandaa kutoa adhabu kali kwa hili shamba la mizabibu: atavunja kwanza kuta zake, atawaruhusu adui walivamie, wanyama wakali waingie ndani yake. Katika mfano huu wa Zabibu kuna hali mbili zinazo pingana: Mungu ambaye anatoa upendo kamili kwa watu, na watu wanao kataa upendo huu kwa kuenenda bila haki ( Isa 1:11-17). Wito huu wa Isaya unaletwa tena kwetu kwa Wakristo leo. Kwasababu ya kukosa uaminifu Israeli watakumbana na ghadhabu kwa taifa lote. Na haya yatawakuta kwa kushambuliwa na mataifa mengine ya njee na kubomoa hekalu lao na kuwa magofu (Is 1:8). Alama hii ni ishara ya upofu wa mtu ambaye anaamua kukataa, makosa yake, kukataa kujirudi na kurudi kwa Mungu.
Kama Nabii Isaya, Yesu pia anatumia ishara ya Ya zabibu kuelezea kazi ya Mungu na majibu ya mwanadamu. Lakini mtazamo upo tofauti. Huyu Mkulima alipanda zabibu na kuzungushia uzio, akajenga mnara na kuwapatia watumwa wake na kusafiri. Wakati wa mavuno ulipotimia akawatuma watumishi wake kwenda kukusanya mavuno, lakini cha kushangaza hawa wakulima hawakutaka kutoa mazao. Huenda walitaka wakusanye mazao kwa ajili yao wenyewe, au pengine hawakuwa na kitu cha kutoa pengine kwasababu hawakufanya kazi. Walianza kushambulia watumishi na kuwapiga hatimaye kuwaua watumishi. Lakini huyu Bwana shamba hakati tamaa bado anawatuma wengine tena na wanawatenda vivyo hivyo, na hatimaye anaamua kumtuma Mwanaye wa pekee lakini bado wale wafanyakazi wa shamba wakamshika na kumua pia. Na hapo wanajiona kwamba wameshinda na kuwa wamiliki sasa wa shamba la mizabibu.
Kama ilivyo katika somo la kwanza, kila ishara iliyopo katika Injili ina maana yake. Bwana Shamba ni Bwana ambaye daima amewapenda watu wake na kuwapa mapendo yote na kuwajali (Mstari. 33). Kuta ni Torati au sheria ambazo Mungu aliwapa watu wake, ili ziwalinde kutoka katika maadui wao, maana yake kuwalinda juu ya tabia isio faa ambayo itawaingiza kwenye hali mbaya. Watumwa ni viongozi wa dini na siasa, ambao kazi yao kubwa ni kuwaongoza watu waishi maisha ya mfano ambayo yatawafanya wazae matunda mema kwa matendo mazuri, kwa upendo kwa Mungu na jirani ambao huyu Bwana shamba anatazamia. Matunda yanatambuliwa na somo la kwanza. Ni kazi ya upendo kwa jirani, upendo na haki. Makundi ya watumishi mawili ni manabii, ambao walitumwa na kuhubiri kabla na baada ya utumwa wa Babeli, mara nyingi sana ili kuwaonya Waisraeli kuwa waaminifu kwa Agano. Mwana ni Yesu.
Kwa njia ya mfano huu Yesu anatabiriwa pia kifo na ufuko wake. Hawa viongozi walimchukuwa Mwana wake wa Pekee na kumtupa njee ya shamba la mizabibu. Na hili ndilo lililotokea kwa Yesu. Aliitwa kuwa ni msaliti wa sheria, alitolewa njee ya mji na kusulubiwa. Lakini Mungu kwa kumfufua, alimtukuza na kumfanya Bwana, jiwe kuu la pembeni la jengo jipya. Kuingilia kwa Bwana shamba ndipo kuna hamisha shamba lile na kupewa wafanyakazi wengine ambao wataleta matunda mazuri. Hii sio matokeo ya Bwana shamba kuchukia, bali ishara yake ya mapendo na kupenda kukomboa. Sio hata kwa kuwaua manabii wake au kumua Mwanaye wa pekee kutamfanya awe adui wa Mwanadamu. Mathayo kwa kuonesha mfano huu alitaka kuonesha jinsi viongozi walivyo wapoteza watu na kumkataa Mwana wa Mungu. Sio kwa wao tuu, bali pia akitazama jumuiya yake na ulimwengu mzima. Kila mwanadamu ni mche wa mzabibu ambao Mungu anategemea kuvuna matunda kwake. Na habari njema kabisa inayo ipamba Injili ni kwamba, pamoja na Mwanadamu kumkataa Mungu, Mungu daima anatafuta njia za kumuokoa na kupata matunda mazuri ambayo anataka kupata.
Sala:
Bwana, nipe hekima na mangamuzi. Ninaomba pia unipe nguvu na neema wakati napaswa nitimize mapenzi yako. Yesu ninakupa maisha yangu Bwana wangu, ninakuamini wewe.
Amina
0 Imependwa
0 Maoni
Maoni
Ingia utoe maoni