Alhamisi. 28 Novemba. 2024

Tafakari

Jumapili, Oktoba 01, 2017

Jumapili, Oktoba 1,  2017,
Juma la 26 la Mwaka

Ez 18: 25-28; 
Zab 24: 4-9; 
Filp 2: 1-11; 
Mt 21: 28-32


KUFANYA MAPENZI YA MUNGU!

Leo Lirtujia ya leo inatualekeza kwenye ujumbe muhumu sana kutimiza mapenzi ya Mungu , yanatufanya sisi tuwe wafuasi wa kweli wa Kristo”. Mwanzoni kabisa mwa tafakari yetu, tufanye ujumbe huu ni wetu kwa kujiuliza maswali yafuatayo. Je, mimi ni mtoto yupi, katika mfano huu, yule anayesema ndio alafu haendi au yule anayesema hapana alafu anaenda?

Baba alikuwa na watoto wake wawili na alitaka watoto wote wamtii. Aliwaagiza wafanye kazi maalumu. Watoto hawa wawili wana tabia tofauti, katika kufuata agizo la Baba yao. Ni vigumu tunakutana na ndugu wawili au mapacha wawili wenye tabia moja. Na hawa wawili walikuwa hivyo hivyo. Wa kwanza mara moja alikubali lakini baadae akabadilisha akili yake. Kwa haraka alikuwa na shauku ya kumsikiliza Baba yake na kufanya kama alivyo agiza. Utayari wake na kwa jinsi alivyo jibu ni hakika. Mara nyingi kushindwa kufanya maamuzi inafanya hali ya uvuguvugu kuingia na hali ya kushindwa hujiingiza. Mtoto wa pili naye anakamatwa katika hali ya kushindwa kuamua. Alikuwa mwazi kwa Baba yake kwamba hawezi kwenda kufanya kazi. Alisema alichokuwa akihisi ndani mwake. Lakini hali ilibadilika tunapo enda upande wa pili wa huu mfano, sehemu ya kuishi na kutenda. Wote wawili waliamua kufanya tofauti, kufanya kile ambacho walikuwa hawajakubali. Na katika kuhamua yule wa kwanza alimkosea Baba yake, lakini wa pili alimpendezesha Baba yae.

Je, hawa watoto wawili katika Injili ni watu wawili tofauti? Ni kweli kwamba ni watu wawili katika mfano au tabia mbili tofauti. Lakini tukiangalia kwa ukaribu kabisa katika maisha yetu, hawa wanaweza wasiwe watu wawili bali hali mbili, njia mbili za kufanya kitu katika mtu mmoja. Watoto hawa wanawakilisha mtu mmoja pia ambaye anafanya vitu tofauti, kuwakilisha mtu ambaye anabadilisha mambo pengine kwa mabaya kabisa au kwa mazuri. Wakati mwingine tunasema ndio na wakati huo huo tunajua tunasema hapana. Na wakati huo kufanya tofauti na kile tulicho sema. Hili linaweza kuwa kweli hasa katika chaguzi mbali mbali tunazo fanya katika maisha yetu ya kila siku na hata chaguzi tunazo fanya mbele ya Mungu, katika kufanya mapenzi yake. Huu mfano tunaweza kuuita mfano wa “waongeaji na wanao tenda”. Wale ambao daima ni waongeaji na wanaweka maisha yao katika maneno hawa ongoki na kufuata mapenzi ya Mungu.

Nabii Ezekieli anawaalika watu waache njia zao mbaya na kumgeukia Mungu, akiwaalika waache dhambi, kutoka katika ulimwengu wa kukosa uaminifu kwa Mungu, waanze kufanya mapenzi ya Mungu. Na ambaye anaacha njia yake mbaya na kutenda mapenzi ya Mungu, anaishi kweli uaminifu. Mstari wa mwisho wa sura hii ambao hatuja usoma leo. Ni mwaliko wa Mungu wa “kuongoka na kuishi”. Yesu hakuhubiri tu mapenzi ya Mungu bali aliyaishi. ‘Ingawaje alikuwa yu namna ya Mungu alionekana kama mwanadamu’ ni maneno ya Mt. Paulo kwa Wafilipi akionesha kujishusha kwa Yesu akitualika na sisi tuwe na hali hiyo ya Yesu. Kwa upande wetu mara nyingi ni “ndio” na hapo hapo hapana. Kwa Yesu ilikuwa daima ndio na ikabakikia ndio na daima itabaki kuwa ndio, kwa mapenzi ya Mungu.

Ujumbe wa leo tuna alikwa kufuata maneno yetu na kuyatenda kadiri ya mapenzi ya Mungu, na kuyafuata. Ni mwaliko wa kuishi kwa uaminifu. Na wale wote wanaosikia Neno la Mungu na kubadilika wanapata tuzo kama vile, watoza ushuru, makahaba na wenye dhambi, walivyo acha dhambi na kupata furaha na Amani.

Sala:
Bwana, nisaidie mimi niweze kuwa msikivu wakati ninavyosema mapenzi yako yatimizwe, nisaidie mimi niweze kubadilisha mawazo yangu mabaya au uchaguzi mbaya na nisaidie mimi kwa neema zako niweze kufanya mapenzi yako matakatifu. Yesu nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni