Alhamisi. 28 Novemba. 2024

Tafakari

Alhamisi, Septemba 28, 2017

Alhamisi, Septemba 28, 2017.

Juma la 25 la Mwaka

Hag 1: 1-8; 

Zab 149:1-6, 9;

Lk 9: 7-9


KUKUWA KIUNDANI ZAIDI NDANI YA KRISTO!

Katika somo la Injili ya leo, tunasikia Herode, akifadhaika baada ya kupata habari kuhusu Yesu. Alama iliyo baki katika dhamiri yake bado inaendelea kumkumbusha kuhusu damu aliyo mwaga ya mtu asiye na hatia ya Yohane Mbatizaji. Sehemu ya pili ya Injili pia inatueleza nini kinacho leta furaha –kumtumikia Bwana, na pia kuwafikia wengine. 


Maisha ya Herodi hayakukosa chochote cha anasa na maisha ya kujiburudisha. Lakini, watu hawakuwa wanaongea kuhusu yeye. Wote walikuwa wakiongelea kuhusu Kristo. Baba Mtakatifu mstaafu Benedict wa XVI alisema “Kanisa linalo tafuta kuwa kivutio na maarufu kuliko yote tayari lipo katika njia isio sahihi, kwasababu Kanisa halifanyi kazi kwa ajili yake binafsi, halifanyi kazi ili kuongeza idadi ya watu na nguvu zake. Kanisa lipo kwa ajili ya kuwatumikia watu. Halijitumikii, halitumikii ili kuwa lenye nguvu, bali, linatumikia ili kumtangaza Yesu Kristo: ukweli mkuu, nguvu kuu ya upendo na msahama unao jionesha kwake na ambao unatokea kila wakati kwa uwepo wa Yesu Kristo” 


Mtazamo wetu pia upo kama wa Herodi. Wengi wetu tunaguswa sana na kinachosema Injili na yote ambayo tunapata kutokana na Imani yetu. Tunasikiliza kwa makini maneno ya Baba Mtakatifu na yote Kanisa linayosema hasa pale ambapo pametokea ukosefu wa haki ulimwenguni. Lakini mara nyingi tumekuwa ni katika hali ya juu juu tu. Haishii kuzama ndani kwa Imani zaidi. 


Tutafakari juu ya Imani yetu ndani ya Yesu. Hivi tunatamani kujua zaidi? Je, tunatafuta utashi zaidi au tunaishia juu ya elimu ya juu juu. Pengine tuna marafiki ambao wanataka kufahamu zaidi kuhusu Yesu, lakini hawana wakuwawezesha kuzama ndani zaidi. Tuwaombee na tumuombe Mungu atutumie sisi kama alivyofanya kwa Yohane Mbatizaji kuleta ujumbe kwa wote waliokuwa wakiutafuta.

Sala:

Bwana, nisaidie mimi niweze kukutafuta wewe katika vitu vyote na kila wakati. Wakati giza linapo nisonga naomba unijalie mwanga wakutambua mwanga wako uliyo ufunua kwetu. Unisaidie kupeleka mwanga huo ulimwenguni kwa walio na hitaji kubwa. Yesu nakuamini wewe.

Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni