Jumatano, Septemba 27, 2017
Jumatano, Septemba 27, 2017.
Juma la 25 la Mwaka
Kumbukumbu ya Mt. Vinsenti wa Paulo
Ezra: 9: 5-9;
Tob 13: 2,4,6-8;
Lk 9: 1-6
KUNGUTA MAVUMBI: NAKUACHA MAMBO YA ZAMANI
Yesu alikuwa amemaliza kuwaambia wafuasi wake juu ya kwenda mji baada ya mji ili kuhubiri Injili/ aliwaambia wasichukue chakula wala nguo ya ziada njiani, bali wategemee ukarimu wa wale ambao wanaenda kuwahubiria. Mwandishi wa Methali anasali “Bwana usinifanye mimi tajiri wala usinifanye maskini” (Methali 30:8), kwasababu tukiwa tajiri sana tunaweza kumsahau Mungu, na hata tukiwa maskini sana, tunaweza kuiba na hivyo kujikuta tunaenda mbali na Mungu.
Ana waambia pia watu wengine hawata wapokea. Aliwaambia wakungute mavumbi ya miguu yao wanapo ondoka katika mji huo. Hili lina maana ya vitu viwili. Cha kwanza, tunapo kataliwa tunaweza kuumia sisi wenyewe, ni rahisi kukaa na kuumia na kuwa na hasiri na matokeo yake kuruhusu kukataliwa kwetu kukaleta madhara zaidi kwetu. Pili, ni njia ya kusema kwamba tunapaswa kusonga mbele daima. Hatupaswi kukaa chini na kuanza kuwaza kwanini wametukataa, bali tunapaswa kusonga mbele na kuendela kuwatafuta wale walio tayari kupokea ujumbe wa Yesu, yaani Injili. Kukunguta mavumbi maana yake ni sehemu ya kusema kwamba siruhusu kukataliwa kwangu kuniumize na kushindwa kwenda mbele. Ni njia ya kusonga mbele na kujiambia kwamba siruhusu niongozwe na mawazo mabaya ya wengine. Ujumbe huu wa Yesu sio kwamba unalenga wale wanao tukataa, bali ni kwanza kabisa kuwatafuta wale ambao watatupokea sisi na ujumbe wa Yesu wa Injili ambayo tunapaswa kuitoa.
Tutafakari juu ya uchungu uliobeba moyoni daima kwasababu ya kukataliwa na wengine. Mungu leo anatuita tuachie, tukungute mavumbi na kuanza kuwatafuta wengine kwa mapendo ili tuweze kushiriki upendo wa Kristo na wao.
Sala:
Bwana, ninapo kutana na kukataliwa na kuumia, ninaomba unisaidie niondoe hasira ambayo naweza kuwa nayo. Nisaidie niweze kuendelea na utume wangu wa mapendo na kuendelea kushirikisha Injili yako nao walio tayari kuipokea. Yesu, nakuamini wewe.
Amina
0 Imependwa
0 Maoni
Maoni
Ingia utoe maoni