Jumatatu. 13 Mei. 2024

Tafakari

Jumatatu, Agosti 15, 2016


Jumatatu, Agosti 15, 2016,
Juma la 20 la Mwaka

Sherehe ya Bikira Maria Kupalizwa Mbinguni.

Ufu 11:19, 12:1-6, 10;
Zab 44:10-12, 16;
1Kor 15:20-27;
Lk 1:39-56


LENGO LA JUHUDI ZETU!

Leo, katika sherehe ya kupalizwa Mbinguni Bikira Maria, Mama wa Mungu, tunasheherekea kupita kwakwe kutoka katika hali ya duniani na kwenda katika hali ya neema mbinguni. Kwa kutafakari utukufu wa Maria Mbinguni, tunaelewa kwamba duniani sio makao yetu ya kudumu , na kama tutaishi maisha yetu yakiwa na matazamio ya maisha yajayo na umilele, ni hakika nasi tutapata nafasi siku moja katika utukufu huu, nahata hivyo kwakuishi kwa matazamio hayo duniani pia patakuwa mahali pazuri pakuishi. Hakika, hatupaswi kupoteza matumaini yetu hata katika matatizo elfu na zaidi yanayo tuzunguka. Mwanga wa Mama yetu aliyepalizwa mbinguni, unaangaza zaidi wakati wa kivuli cha huzuni na mateso yanapokuja katika njia zetu.

Kupalizwa tunasherehekea tukio moja la Bikira kushiriki katika ufufuko wa Mwanaye ambapo kwahiyo alichukuliwa mbinguni kwa utukufu mwili na roho wakati maisha yake yalipoisha hapa duniani. Ni hakika, ujumbe wetu kwa tukio la kupalizwa Bikira Maria unatupa kile ambacho sisi tunapaswa kutarajia wakati ufufuko wetu utakapotokea siku ya mwisho. Kupalizwa kwa Mama ni kikomo cha kweli cha wote walio katika Kristo. Kama mtakatifu Paulo anavyotuambia, tutafufuliwa katika wafu tukiwa na miili yenye utukufu kama ule mwili wa Kristo mwenyewe. Kwanjia za nguvu ya utukufu wa Yesu mfufuka, nasi tutapata ukamilifu wote kwa Mungu katika utukufu wa Kristo, kama Maria alivyopata katika kupalizwa.

Katika siku hii ya kupalizwa Mama, ni siku ambayo tunaitwa tutafakari kuhusu lengo letu la baadaye na matumaini katika utukufu. Kwahiyo mambo yetu yote yawe katika njia hii na yaangukie katika njia hii. Tunapaswa tujioni sisi tukisimama kama Maria katika utukufu, tukivikwa utukufu ung’ao kama jua na taji la nyota juu ya vichwa vyetu. Katika somo la ufunuo tunaona taswira ya Mama ambapo katika uhalisia kamili, mama huyu ni Kanisa la Mungu ambalo ndio bi harusi wa Kristo mwenyewe, ndani ya kanisa utukufu wote wa Kristo upo, na kwanjia ya kanisa watoto wake wanazaliwa kila mara wakati mwingine katika uchungu, nyoka yule ndiye muovu amejaribu kuharibu watoto wa Mama Kanisa huyu lakini kwa njia ya Kristo Mungu hulitegemeza kanisa la Mungu licha ya nyakati ngumu na misukosuko linalopata wakati mwingine. Tunapaswa tuendelee kutenda mema ili nyoka huyu (muovu) aweze kutupwa njee ya njia zetu, tunapaswa tuwatafute wenzetu na kusaidiana sisi kwa sisi, kwanjia ya neema na kwanjia ya msaada wa Mama Maria, tuzae matunda, hata wakati mwingine katika uchungu, maisha yetu yakiwa ndani ya Kristo. Kwa njia hii, ufufuko wetu, mwili na roho utakuwa hakika, na maisha yetu yatachukua na kupata maana halisi na tutatambua ukweli ulipo katika dogma ya Bikira Maria kupalizwa mbinguni ni hakika ya tamaa yetu ya ndani kuhusu maisha yetu.

Sala: Ee mwenye huruma na mpendwa Mama, tunaomba uzuri wa utukufu wako uliopewa na mwanao utuombee nasi tujazwe mioyoni mwetu ili tusiweke mioyo yetu katika mambo ya ulimwengu huu, bali tuwe na tamaa daima ya kutarajia utukufu wa mbinguni. Amina

Maoni


Ingia utoe maoni