Jumapili, Septemba 24, 2017
Jumapili, Septemba 24, 2017,
Juma la 25 la Mwaka
Isa 55: 6-9;
Zab 144: 2-3,8-9,17-18;
Phil 1: 20-24, 27;
Mt 20: 1-16
SI HAKI YAKO, BALI NI NEEMA!
Liturjia ya leo inatupa hali ya kivutio kizuri sana kuhusu Mungu. Inautambia kwamba Mungu hayupo katika hali ya ubaya au ugumu kama sisi tunavyo fikiri. Yeye ni mkarimu, mwenye huruma, na mwenye kusamehe. Yeye ni mkarimu na mwingi wa huruma, hakasiriki upesi ni mwingi wa mapendo.
Sisi mara nyingi tunamtazama Mungu katika hali ya ubinadamu. Tunamfanya awe katika hali ya udogo na fikra kama za kwetu. Lakini katika somo la kwanza kutoka kitabu cha nabii Isaya, Mungu anasema “njia zangu sio njia zenu”. Waisraeli walipokuwa utumwani huko Babiloni waliteseka sana. Kwa machozi wazee wa Waisraeli waliwaelezea kizazi kilicho zaliwa huku utumwani kwa machozi jinsi hekalu lao la Yerusalemu lilivyo bomolewa, wakiwaonesha ni kwa jinsi ghani Mungu alivyo waacha. Wakimuonesha Mungu kama Mungu anaye lipa kisasi, anaye wakirimia wanaotenda mema na kuwa adhibu walio wabaya. Katika hali hii, Isaya anasema na kuwapa maneno mengine tofauti na fikra zao; njia za Mungu sio kama za wanadamu. Nabii anawaambia wabadilishe mtazamo wao kuhusu Mungu. Badili njia zote mbaya ambazo mwanadamu anaonesha kwamba Mungu anazo. “mawazo yangu sio sawa na mawazo yenu, njia zenu si sawa na njia zangu. Kama vile mbingu zilivyo mbali na nchi, ndivyo njia zangu zilivyo mbali na mawazo yenu”.
Somo la pili linabeba mistari aliyo andika Paulo akiwa gerezani kwa ajili ya watu wa Filipi. Anafikiria huhusu kifo chake lakini anakumbuka kuhusu muunganiko kamili na Kristo. Katika mistari hii anafunua hali nzuri ya moyo wake. “kwangu kuishi ni Kristo, na kufa ni faida” ni muunganiko wa hisia zake na Imani yake.
Somo la Injili linabeba simulizi kuhusu ukarimu wa Mungu, ukarimu ambao unapanda juu zaidi ya ukarimu wetu wa kibinadamu. Huu ni mfano wa ajabu kabisa . mfano huu unawafanya wasikilizaji kukasirika. Ni nini maana ya mtu kujituma na kutimiza majukumu yake yote wakati mwishoni tunakuja kulipwa sawa na wengine? Ya nini kujishughulisha siku nzima wakati wengine wanakuja saa kumi na moja jioni na kupokea mshahara sawa na wewe uliye anza saa moja asubuhi?
Ni vizuri kutambua kwamba wale waliokuwaja saa kumi na moja hawakuwa watu walio lala tu bali walikuwa watu ambao walikuwa wakitafuta kazi katika hali zote, na wala hakuwa watu wakukwepa kazi. Walikuwa katika hali ya kweli kutaka kufanya kazi. Ni kwamba hawakupata tu mtu wa kuwaajiri. Kipindi hicho sehemu ya soko ilikuwa ndio sehemu ya kutafutia ajira. Watu walienda pale, wakisubiri mtu aje na kuwaajiri. Kama mtu alihitaji watu wa kuajiri alienda tu sokoni na kupata watu, lakini ilipofika saa kumi na moja hakuna mwajiri hata mmoja aliye waajiri, lakini walikuwa tayari kufanya kazi.
Sasa kila mtu alifahamu ni nani Yesu anamuongelea katika Injili. Wale watu wa saa kumi na moja walikuwa ni wadhambi na Wayunani. Wale ambao walikuwa wakifanya kazi mchana kutwa walikuwa Waisraeli. Na shamba lilikuwa ni ufalme wa Mungu. Aliye waajiri ni Mungu. Yesu alikuwa anasema kwamba Mungu amewapa ufalme wake wadhambi na Wayunani sawa sawa na Waisraeli. Katika hali halisi Wayahudi walipinga sana. Hawakudhani kwamba ni haki, walidhani kwamba wanahitaji mshahara maalumu kwani walikuwa wakifanya kazi muda wote wamekuwa na Mungu katika maisha yao. Lakini Yesu anabadili mtazamo wao waliokuwa nao tangu kuzaliwa.
Ukarimu ni kitu pekee kilicho hitajika kwani kilifanya watu wote kupokea sawa. Iliondoa hali yao ya kujiona wema na kwamba wanahitaji ukarimu maalumu. Walidhani kwamba Mungu anapendelea. Wakidhani kwamba Mungu atawapa zaidi kwasababu ya kazi ngumu waliofanya. Yesu anaweka mtazamo mpya kwamba Mungu ni mkarimu kwa watu wote. Yesu anamuonesha Mungu kama Baba mwenye huruma. Yeye ni Baba yetu wa Mbinguni, sisi ni watoto wake. Ni wazi kwamba Baba anapaswa kuwa mkarimu kama anahitaji jina hili katika uhalisia wake. Mfano huu unonesha hali halisi kwamba Mungu ni mkarimu. Ukarimu wake upo kwa ajili ya watu wote, hata kwa wadhambi na Wayunani. Hatupaswi kumfikiria Mungu kuwa yupo kama sisi. “mawazo yangu sio sawa na mawazo yenu”, asema Bwana.
Kwa wakristo tunachopaswa kutazama sio taji au malipo, bali furaha ya kumtumikia Mungu. Sio tu kitu kizuri kufanya kazi katika shamba la Mungu, bali ni thamani kubwa, badala ya kubaki katika soko siku nzima, bila maana hali ya maisha. Kama Mungu anawaonea huruma wale ambao siku nzima wamekuwa wakitazamia kuajiriwa na kuwachukuwa na kuwapa thamani ile ile kama sisi na kuwakirimia sawa na sisi, kwanini kukasirika? Hili linatufundisha kitu. Kama tunakasirika basi tujue kwamba kuna kitu kinapungua katika maisha yetu ya kumtumikia Mungu. Kuna ubinafsi ndani mwetu, au pengine hatufanyi kazi kwa ajili ya Bwana bali tunafanya kwa ajili yetu. Au pengine, huenda hatujaacha ile tabia ya kujiona wenyewe kuwa wema na kujipa utukufu kwasababu tunatenda matendo mema.
Njia nzuri ambayo tunaweza kufanya na kuwavutia wote ni kufanya kila kitu kwa upendo. Ingawaje sio rahisi, lakini hili ndilo linalo kirimu katika hali ya ukubwa kabisa. Ni katika moyo huu tunaweza kufanya katika hali njema na haki. Kama moyo wangu haupo kwenye kazi basi mimi sina tufauti na mtumwa. Lakini kama moyo wangu upo ndani yake, inakuwa ni furaha na ninaweka jitihada yangu yote ndani ya kazi. Kufanya kazi kwa mikono tu, bila kuwa na moyo haina tofauti na mtu ambaye hana mikono. Hivyo tuvae upendo na tutambue Mungu ni mkarimu kwa watu wote na anapenda watu wote waonje huruma na ukarimu wake, Mungu hafurahii muovu kupotea bali aache njia yake na kuonja ukarimu na huruma yake. Mwenzako anavyorudi kutoka kwenye dhambi furahi na mtukuze Mungu, usinune na kuanza kutafuta njia ya kumrudisha kwenye dhambi.
Sala:
Bwana, nisaidie mimi niweze kuongeza bidi katika kuishi maisha yangu ya Imani. Nisaidie mimi niweze kusikia sauti yako na wito wako wakunialika nifanye kazi katika shamba lako la neema. Ninakushukuru wewe kwasababu ya ukarimu wako na huruma yako unayotupatia kama zawadi kwetu. Yesu nakumini wewe.
Amina
0 Imependwa
0 Maoni
Maoni
Ingia utoe maoni