Jumatatu. 13 Mei. 2024

Tafakari

Jumamosi, Agosti 13, 2016

Jumamosi, Agosti 13, 2016,
Juma la 19 la Mwaka

Ez 18:1-10, 13, 30-32;
Zab 50:12-15, 18-19;
Mt 19:13-15

SOMO KUTOKA KWA WATOTO!

Leo somo la Injili kwa ufupi linaelezea jinsi Yesu alivyo wakubali watoto. Wafuasi wanawazuia watoto, pengine ni kwasababu ya sheria ya kujiweka safi. Watoto wadogo katika hali walizokuwa wakiishi ilikuwa inachukuliwa kuwa sio safi, rahisi kuchafuka. Kama walitaka kumgusa Yesu wangemchafua pengine. Yesu hajali hiyo kuhusu sheria ya usafi isiyojali undugu na kumrusu kuwa na wadogo. Upya katika Mungu, Baba aliye ndani ya Yesu anayaweka alama maisha ya Yesu na anampa macho mapya ya jinsi ya kutufundisha kuthamini na kujali uhusiano kati ya watu. Yesu anakuwa upande wa watoto waliotengwa na anakuwa mlinzi na kinga kwao.

Inavutia sana kuhusu Biblia na hasa tabia ya Yesu kuwajali watoto na kuwalinda, watoto wanaelewa kuhusu mambo ya Ufalme aliotangaza vizuri zaidi kuliko wale waliojiona waelewa. (Mt 11:25-26). Wanapokea bila kubadili maana na kukwaza. Kati ya maneno makali ya Yesu ni kuhusu wanaosababisha makwazo kwa walio wadogo, akimaanisha wale wanaosababisha wadogo wasiwe na Imani kwa Mungu. Kwasababu ya hili, ni bora wangefungwa jiwe la kusagia shingoni na kutupwa baharini (Lk 17:1-2; Mt 18:5-7). Yesu anawataka wafuasi wawe kama watoto wadogo ili waweze kuupokea Ufalme kama watoto wanavyopokea. Bila kuwa hivi, itakuwa vigumu kuingia kataka Ufalme wa Mungu (Lk 9:46-48). Ina maana kwamba watoto wamefanywa kuwa walimu wa wakubwa. Watoto ni wanyofu daima, wanawategemea wazazi bila kuwa na wasiwasi, sisi nasi tumtegemee Mungu bila kuwa na wasi wasi tukiwa na mioyo minyofu kama watoto.

Sala: Tusaidie Ee Baba kuwa kama watoto katika uhusiano wetu nawe. Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni