Jumatano, Agosti 30, 2017
Jumatano, Agosti 30, 2017
Juma la 21 la Mwaka
Sala ya Kanisa (Zaburi) - Juma 1
___________________
MASOMO YA MISA
1 Thes 2: 9-13;
Zab 138: 7-12;
Mt 23: 27-32.
___________________
KUONDOA UFARISAYO NDANI MWETU!
Katika somo la Injili leo Yesu analalamika na kusema ole juu ya Mafarisayo na Waandishi kwasababu ya hali yao ya unafiki. Walikuwa wamewabebesha watu mizigo ya sheria na mambo ya njee. Waliwatesa na kuwadhulumu manabii waliokuwa wajumbe wa Mungu na kukataa kusikiliza sauti ya Mungu waliokuwa nayo ndani yao juu yao na watu wote. Wamefana na makaburi yaliopakwa chokaa, yanayo onekana mazuri kwa njee lakini ndani yamejaa mifupa na uozo. Mafarisayo na waandishi walionekana wenye haki mbele za watu lakini hawakuweza kukukutana na mwenye haki Mwenyewe-Yesu.
Kitu kimoja muhimu ni kwamba Yesu ni mwaminifu mno. Wewe je? Upo tayari kufanya kila kitu kwa uaminifu wote? Je, upo tayari kuwa mwaminifu mbele ya Mungu na juu ya roho yako mwenyewe? Tatizo ni kwamba hatuoni hivyo. Daima tunajipitisha mbele ya watu tukijifanya kwamba ni wema na kukwepa ukweli wa mifupa na kila aina ya uchafu uliyo ndani mwetu. Hili sio jambo zuri na Yesu analipinga hili katika Injili.
Leo Injili inakualika utazame ndani ya moyo wako katika hali ya kweli, na ujiulize unaona nini? Natumaini utaona wema na fadhili na kuzifurahia. Lakini pia katika hali ya kweli utaziona dhambi. Pengine sio katika hali kama ya Mafarisayo, lakini kwa hakika utaona hali ya dhambi ambazo zinapaswa kusafishwa. Tafakari leo, ni jinsi ghani waweza kuzitazama dhambi zako katika hali ya kweli na jinsi ya kuziacha.
Sala: Bwana, nisaidie mimi niweze kuchukua hatua ya kujitazama mimi mwenyewe maisha yangu. Nisaidie nisione tuu fadhila nzuri ulizoweka ndani yangu, lakini pia nisaidie niweze kuona uovu au dhambi zilizo ndani ya moyo wangu. Ninakuomba unisafishe kutoka katika dhambi hiyo ili niweze kukupenda wewe zaidi. Yesu, nakuamini wewe. Amina
Maoni
Ingia utoe maoni