Alhamisi. 28 Novemba. 2024

Tafakari

Jumapili, Agosti 27, 2017

Jumapili, Agosti 27, 2017
Juma la 21 la Mwaka
___________________

Isa 22: 19-23;
Zab 137:1-3, 6, 8;
Rum 11:33-36;
Mt 16:13-20
___________________

NINYI MNASEMA MIMI NI NANI?

Picha ya Yesu inayotumika kwa tangu miaka 2000 iliyopita, anatumika kama rafiki wa waliotengwa, mwenye ujumbe ulioleta mapinduzi katika maisha ya Mwanadamu, mshindi wa falme mbali mbali na mlinzi wa viongozi. Yesu tabia yake ni tabia ambayo kila mmoja anapenda kufanana nayo au kuishi kama yeye. Sisi pia tuna picha ya Yesu ambayo tunabeba ndani mwetu tangu tukiwa wadogo. Baada ya miaka yote hiyo hajawahi kumuuliza mtu kama alivyo fanya karibu na Kaisaria Philipi, “Ninyi mnasema mimi ni nani?”

Katika somo la kwanza kutoka katika kitabu cha nabii Isaya, mfalme Hezekia amemchagua Shabna kama mkuu wa nyumba yake. Shabna, mtu wa kutafuta maslahi na mtu wa kupenda rushwa, aliye kinyume na ujumbe wa nabii Isaya anafanya njama na Wamisri. Shebna anaondolewa na Eliakimu, mtu mwaminifu, mwenye uwezo, wakutegemewa katika siasa. Eliakimu alikuwa mevikwa koti la mtangulizi wake, akapewa mamlaka yote na hatimaye akapewa ufunguo na kuwa na nguvu zote juu ya ufalme.

Katika somo la Injili, Yesu anawauliza mitume maswali mawili. La kwanza ni rahisi “Je, watu wanasema Mwana wa Adamu ni nani? Na swali la pili linalo leta changamoto ni “nyie mnasema mimi ni nani?” Yesu aliwaheshimu watu wote wa zama zote na muda wote. Amekuwa ni kiungo cha kupendwa na kutukuzwa. Lakini Yesu hakufuata ujanja wa kibinadamu na mitizamo yao. Aliyapa kipaumbele maisha ya Kimungu, taratibu huku akifunua mpango wake, na baadae kushinda werevu wa mwanadamu na ufahamu wake kwa katika maisha yake mwenyewe. Wafuasi wake hawakuwa wafuasi kwasababu tu walimfuata. Mfuasi wake ni yule aliye elewa kwamba yeye ni wa pekee, yeye ambaye amempenda kwa moyo wote, kumwamini kabisa na kuwa tayari kufanya chochote kwa ajili yake. Ni katika hali hii Petro anakuja na jibu la pekee. Alisema “wewe ni Masiha” Mwana wa Mungu aliye hai, ambaye Manabii walikutabiri na ambaye una tazamamiwa.”

“Wewe ni ambaye sisi tumeamua kujitoa maisha yetu kwa ajli yako.” Petro alitoa jibu zuri sana lakini katika maneno tu, lakini katika akili yake alikuwa na wazo tofauti. Alikuwa na hakika kwamba Yesu alikuwa anakaribia kuanzisha ufalme wake hapa duniani na hivyo angetumia nguvu, miujiza mikali na mambo mengi ya kushangaza ambayo yataleta mshangao na kuvuta hisia za watu. Haya pia yalikuwa ndio matazamio ya wafuasi wengine, licha ya wao kufahamu kitu tofauti na makutano wamefungwa na mawazo ya kizamani bado.

Katika sehemu ya pili ya Injili Yesu anamwambia Simoni Petro: “Wewe ni Petro na juu ya Mwamba huu nitalijenga kanisa…” . Maelezo ya maneno haya ni magumu zaidi ya jinsi tunavyo yatazama. Kwanini na kwasababu ghani Simoni Petro anaitwa Mwamba ambao juu yake atalijenga kanisa? Kwanza kabisa, tunatambua kuwa “mwamba” kama msingi wa kanisa umeongelewa pia sehemu nyingine katika Agano Jipya. Mwamba huu, ambao ni mgumu usio sogea, daima ni “Yesu Kristo” hakuna mwigine -Paulo anasema hakuna anayeweza kuweka msingi mwingine tofauti na ule ambao umewekwa, ambao ni “Yesu Kristo” (1 Kor 3:11). “ninyi ni nyumba ambayo misingi yake ni mitume na manabii, na jiwe kuu ni Kristo mwenyewe..” (Ef 2:19-21). Petro pia katika barua yake anawaalika wabatizwa wapya wasijitenge kabisa na Kristo kwani yeye ni “jiwe””mwamba” unao ishi, uliokataliwa na watu, lakini aliyechaguliwa na mwenye thamani machoni pa Mungu (1 Pet 2:4-6). Sehemu ya pili ni kwamba jina alilolopewa Simoni kama Kefa au Petro katika lugha ya Aramaiki katika hali zote halina maana ya “mwamba” bali jiwe la kujengea. Jiwe analosema Yesu ni Imani inayotangazwa na Petro. Imani ambayo imebeba msingi wa kanisa, ambayo inalifanya liunganike na “Kristo-Mwamba”, na kulifanya lisiharibiwe na kulifanya lisiguswe na nguvu za yule muovu. Wale wote kama Petro, wanao amini na kutangaza Imani hii, tumewekwa kama mawe hai, katika nyumba ya kiroho alioijenga Mungu mwenyewe.

Petro pia alipokea funguo za kufunga na kufungua. Kumpa mtu ufunguo ni kumwamini kwamba ataweza kazi unayompa. Marabii au walimu wa sheria walidhani kwamba wameshika “ufunguo wa Torati” kwasababu waliyafahamu maandiko. Waliamini kwamba kila mtu lazima alikuwa awategemee. Maamuzi yao. Yesu anachukua usemi huu katika hali ya ukali “lawama ipo juu yenu ninyi walimu wa sheria, kwani mmechukua ufunguo wa akili. Ninyi wenyewe mmeshindwa kuigia na mmewafungia wengine wasipate kuingia” (Lk 11:52). Badala ya kufungua milango ya wokovu watu waingie wameifunga watu wanashindwa kuingia badala ya kuwangulia watu ukweli kuhusu Mungu na mapenzi yake. Yesu anawa nyanganya ufunguo ambao wenyewe waliutumia vibaya. Na sasa ni hivi “Ufalme wa Mbinguni” ni wazi kwa wafuasi wote wanaopenda kuingia na ufunguo wa kuingia ni Imani iliotangazwa na kukiriwa na Petro. Kwa kumpa Petro ufunguo haina maana kwamba anamfanya Petro kuwa mlinzi wa mlango wa kuingia mbinguni. Bali Yesu anamwambia “yeye awe mfano kwa kundi” (1 Pet 5:3). Anamwamini yeye afungue zaidi akili ya ufahamu wa Kristo na Injili yake. Wanaopita kwa kutumia mlango uliofunguliwa na Petro kwa kutangaza imani anayo ikiri atapata wokovu, anaye ikataa basi anajifungia mwenyewe.

Wakti Yesu alivyo uliza “watu wanasema mimi ni nani” (Mt 16:13), si kwamba ni kwasababu alikuwa anataka kufahamu kuhusu sura yake. Ni kutaka kujua kama mtazamo wa watu unaendana na ukweli wenyewe kuhusu yeye –kama wanamfahamu kweli. Jibu linalo tolewa linaonesha kwamba watu hawakuwa sahihi. Lakini Yesu yeye anataka kubaki mwaminifu katika utume wake kama Kristo. Nia moja tu ambayo alitaka kutimiza ilikuwa ni nia ya Baba yake “chakula changu ni kutimiza mapenzi ya Baba yangu” (Yn 4:34).

Katika muda mmoja au mwingine, sisi pia tunapaswa tuelezee Yesu ni nani katika maisha yangu. Tujaribu kuelezea leo na kuangalia kuhusu Imani yetu na uelewa wetu kuhusu Kristo, Masiha. Tutafute kutambua “siri” ya utambulisho wake halisi tukisikiliza sauti ya Baba yetu anaye ongea nasi ndani ya mioyo yetu. Ni katika moyo huu tunaweza kuingia katika Imani ya kweli kuhusu Mwana wa Mungu. Tuvutwe katika hali ya kuwa na Imani na kumvaa Yesu Kristo, ili tuweze kutangaza Imani, kwani hili ndilo la maana katika wito wetu wa Ukristo tulio uvaa. Ni kwa njia ya Imani tu ndani ya Kristo tunaweza kungara na kuwa na nguvu dhidi ya yule muovu na kumshinda.

Sala: Bwana, nina amini kwamba wewe ni Kristo, Masiha, Mwana wa Mungu! Nisaidie kukosa Imani kwangu ili niweze kukuamini wewe na kukupenda kwa nafsi yangu yote. Yesu nakuamini wewe. Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni