Jumatatu. 13 Mei. 2024

Tafakari

Alhamisi, Agosti 11, 2016

Alhamisi, Agosti 11, 2016,
Juma la 19 la Mwaka C wa Kanisa!

Kumbukumbu ya Mt. Clara, Bikira.

Ez 12: 1-12;
Zab 77: 56-59, 61-62;
Mt 18: 21-19:1


MSAMAHA KATIKA MAISHA YA MKRISTO!

Inasemwa kwamba kukosea ni ubinadamu lakini kusamehe ni Umungu. Kwa njia hii kusamehe imekuwa changamoto kwa mwanadamu. Katika Injili, jibu la Yesu lipo tofauti na mawazo aliyokuwa akiwaza Petro, kwamba kusamehe hakuna kikomo. Inapaswa kuendelea na kuwa hali halisi katika maisha ya mtu.

Msamaha hautufanyi dhaifu, wajinga, kudhalilika, au wasio na thamani. Bali unatualika katika hali ya juu kabisa ya kuishi. Kwanza kabisa maisha ya Bwana yalikuwa maisha ya msamaha. Aliwasamehe wafuasi wake na adui zake. Zaidi sana, anatusamehe sisi na wale waliotukosea. Kwahiyo, huwa tunamuomba kila tusalipo sala ya Baba yetu, “atusamehe dhambi zetu kama tunavyo wasamehe waliotukosea”. Ulimwengu hauwezi kusitawi kama tutatafuta tu haki. Hamna Amani kama hamna haki kadhalika hamna haki kama hamna msamaha.

Ya pili, msamaha si sawa na kusahau; bali msamaha ni sawa na utakatifu. Msamaha hauwezekani bila neema ya Mungu. Naweza tu kuwasamehe adui zangu kama kuna neema ya Mungu ndani mwangu-maisha binafsi ya kuhisi msamaha wa Mungu ndani mwangu, na ile hamu ya kuwasamehe walionikosea. Kwahiyo, ninaposamehe sisahau kile alichofanya Mungu kwangu.

Na mwisho kabisa, kusamehe sio ubinadamu, ni Ukristo. Leo, Yesu anatualika tufuate hatua alisowafundisha wafuasi wake: ongea na Baba kwanza, ungama sehemu yako, kabiliana na tatizo lenyewe sio kumshambulia mtu, ona huruma na wengine na kuwa muelewa, na baadae chukua hatua ya kuonana na aliyekukosea. Hakuna hatua rahisi katika msamaha. Yesu hakusema itakuwa rahisi katika kumfuata. Msamaha unatupa changamoto sisi wote. Lakini hiki ndicho kinacho tutambulisha sisi na Yesu. Tumuombe Yesu atupe neema yakuachia yote moyoni mwetu na kuwasamehe wote waliotukosea katika maisha yetu yote. Hata kama ni kosa kubwa kiasi ghani, tuachie yote ili Mungu aendelee kutusamehe na sisi na kutupatia Baraka zake.

Sala: Bwana nisaidie niweze kuwasamehe ndugu zangu wote. Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni