Alhamisi, Agosti 17, 2017
Alhamisi, Agosti 17 2017
Juma la 19 la Mwaka
Yosh 3: 7-11, 13-17;
Zab 114: 1-6;
Mt 18: 21-19:1
MSAMAHA KATIKA MAISHA YA KIKRISTO!
Injili ya Leo inaanza na swali la Petro alilomuuliza Yesu kuhusu ni mara ngapi anapaswa kusamehe. Wakati Petro akipendekeza mara saba, Yesu anajibu tena mbali zaidi kwa kusema saba mara sabini. La muhimu sio kuhusu ni mara ngapi bali ni kuhusu msamaha wa kweli kutoka ndani. Kama mmoja atakuwa anahesabu ni mara ngapi amesamehe ni wazi kwamba sio msamaha wa kweli. Mfano unaofuata kuhusu Mfalme anayemsamehe mtumishi anaye mdai talanta kumi na mtumishi huyo huyo akiwa anamdai mwenzake kiasi cha dinari tuu, inaleta maana hiyo hiyo. Tunategemea kusamehewa na wengine tunapo wakosea na kusema samahani. Tunapaswa kugeuzia kwetu hali hiyo hiyo wengine wanapo tukosea na sisi.
Msamaha hauna kikomo. Unapaswa kuendelea na kuwa ukweli wa maisha yetu. Msamaha hautufanyi dhaifu, wajinga au wasio na thamani. Bali unatuita kuingia kwenye maisha ya juu zaidi. Kwanza kabisa maisha ya Yesu yalikuwa maisha ya msamaha. Aliwasamehe wafuasi wake na maadui wake. Cha muhimu yeye anatusamehe sisi na wale waliotukosea, kama tunapo Sali mara nyingi katika sala ya “Baba yetu”, “utusamehe sisi kama tunavyo wasamehe waliotukosea”. Dunia haiwezi kusimama kama tutatafuta tu haki bila msamaha. Hakuna Amani kama hamna haki na hamna haki kama hamna msamaha.
Pili msamaha sio sawa na kusahau, msamaha ni sawa na utakatifu. Msamaha hauwezekana bila neema ya Mungu. Ninaweza kuwasamehe ndugu zangu tu pale kama nina neema za upendo wa Mungu-uzoefu wa kupokea msamaha binafsi kutoka kwa Mungu, na hamu ya kuwasamehe wote walionikosea mimi. Hivyo, ninavyo samehe sisahau kile kitu alicho nitendea Mungu.
Na mwisho kabisa, kusamehe sio ubinadamu, ni Ukristo. Leo, Yesu anatualika tufuate hatua alisowafundisha wafuasi wake: ongea na Baba kwanza, ungama sehemu yako, kabiliana na tatizo lenyewe sio kumshambulia mtu, ona huruma na wengine na kuwa muelewa, na baadae chukua hatua ya kuonana na aliyekukosea. Hakuna hatua rahisi katika msamaha. Yesu hakusema itakuwa rahisi katika kumfuata. Msamaha unatupa changamoto sisi wote. Lakini hiki ndicho kinacho tutambulisha sisi na Yesu. Tumuombe Yesu atupe neema yakuachia yote moyoni mwetu na kuwasamehe wote waliotukosea katika maisha yetu yote. Hata kama ni kosa kubwa kiasi ghani, tuachie yote ili Mungu aendelee kutusamehe na sisi na kutupatia Baraka zake
Sala: Bwana, ninakuungamia kwa kuwa mkaidi woyoni. Ninaungama ugumu wangu wakuto kusamehe. Kwa huruma yako nisamehe mimi na jaza moyo wangu na huruma yako juu ya wengine. Yesu nakuamini wewe. Amina
Maoni
Ingia utoe maoni