Alhamisi. 28 Novemba. 2024

Tafakari

Alhamisi, Agosti 10, 2017

Alhamisi, Agosti 10 2017
Juma la 18 la Mwaka

Sikukuu ya Mtakatifu Laurent, Shemasi na Shahidi

2Kor 9: 6-10;
Zab 112: 1-2, 4, 9 (K) 5;
Yn 12: 24-26.


MBEGU YA AMANI

Yesu Kristo leo anafundisha kwa kutumia mfano wa “mbegu” ambao tuliweza kueleweka kwa urahisi sana. ili mbegu yeyote ipate kuota italazimika ibadilike hali yake ya awali, ipate hewa, maji, mwanga na mazingira yatakayoiwezesha kuoza, ikiwa inabadili hali yake ya awali ndipo tunaona mizizi inaota na majani yanatokeza, taratibu unamea, unakua na baadaye unatoa matunda au mbegu zinazofanana na ile iliyooza. Katika historia ya maisha ya Ukristo tunaambiwa ni kwa damu ya mashahidi. Kanisa la mwanzo lilikua na kustawi na kufikia hali iliyo nayo sasa miaka elfu mbili iliyopita. Kwa ufupi tuna msemo: "Damu ya mashahidi ni mbegu ya Kanisa." Mashahidi ni wale waliouawa kwa kile walichokiamini, wakakitetea yaani imani moja kwa Yesu Kristo. Wale wote waliomwaga damu yao akiwemo Mt. Laurenti wanalinganishwa na mbegu ambayo inakuwa kama imekufa lakini baadaye inazaa sana. Mashahidi wa Kanisa Katoliki waliifia imani aliyotuachia Bwana wetu Yesu Kristo na kwa kifo chao watu wengi pia waliamini mafundisho ya Kristo. Leo, Kristo anatualika sote tuyatoe maisha yetu kuikiri imani yetu, kumkiri Kristo, Tuwe tayari kupinga yale yote yasiyoendana na mpango wa Mungu, tupate kuzaa matunda yaliyo safi na ya kudumu tupate kuishi uzima wa milele na tuwe naye siku zote.

Sala: Ee Bwana, Naomba kuwa mbegu ya Imani, Amina

Maoni


Ingia utoe maoni