Jumatatu, Agosti 07, 2017
Jumatatu Agosti 7, 2017
Juma la 18 la Mwaka
Hes 11:4-15;
Zab 81: 11-16 (K) 1;
Mt 14: 13-21.
KUMTAFUTA MUNGU KATIKA NYAKATI ZENYE KUCHUKIZA!
Leo tunasikia juu ya Yesu kwenda sehemu ya faragha, na kuwalisha watu. Kifungu kimetuchukuwa mbali kutoka katika tukio la kifo cha Yohane Mbatizaji kilicho sababishwa na Herode. Kupanda katika chombo yeye mwenyewe, anakwenda mpaka sehemu tulivu ili kupata muda wa kufikiri….kutafakari na kupata nguvu.
Yesu anachagua sehemu iliyojitenga sio kwa lengo la kujificha bali kuzishughurikia huzuni zake na kutafuta nguvu kwa nyakati zenye kuchukiza. Kujiweka katika sehemu iliyojitenga, sehemu yenye ukimywa hivyo ndivyo tunavyopaswa kufanya wakati tunapohangaika na Imani, na maisha kwa ujumla, na katika huzuni kwa ujumla. Huko ndiko tunakokwenda kulia, kupiga kelele, kupotea, na kutafuta majibu. Kupata jibu katika maswali haya haitoshi tu kuwa pekee katika sehemu iliyojitenga; lakini muhimu zaidi lazima kuwepo kutaniko na Mungu na sehemu iliyojaa uwepo wa Mungu.
Sehemu ya pili kwa asilimia fulani inahusiana na sehemu ya kwanza. Yesu, anayaona mahitaji ya watu na husikia kilio chao. Hakuna mtu aliyeondoka bila ya kushibishwa. Mungu yupo zaidi tunapohangaika. Je, nipo katika jangwa nikitafuta majibu?
Sala: Bwana, njoo katika msaada wangu. Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni