Kutenda Kisichowezekana
· na Shajara Administrator
Petro alikuwa mtaalamu wa kuvua samaki na aliifahamu bahari vizuri sana. Lakini leo, aliambiwa afanye kitu kilichozidi kazi ya utaalamu wakejuu ya maji! “Yesu aliwasihi wafuasi wake waingie mashuani”, alikuwa na ufahamu kuwa maji hayakuwa shwari, wakati mwingine Yesu anaamua kutuongoza sisi katika changamoto au katika hali ngumu, na yeye anasababu kwa hayo. Ili kutembea juu ya maji, Petro ilimpasa atoke nje ya mashua. Wakati Yesu anapotutaka sisi tutende kitu kikubwa sana maishani mwetu, anatutarajia sisi tupige hatua mbali na hali yetu ya sasa ili tujawe na imani, vitu vikubwa. Mpaka tutakapojawa na ujasiri kutoka nje ya mashua na kumuamini Bwana, hatuwezi kutenda kitu.
Sala: Nipotayali kuzifuata Amri zako, Ee Bwana, Amina
Sala: Nipotayali kuzifuata Amri zako, Ee Bwana, Amina
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni