Jumamosi. 23 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatano, Agosti 10, 2016

Jumatano, Agosti 10, 2016,
Juma la 19 la Mwaka

Sikukuu ya Mt. Laurent, Shemasi na Shahidi.

2 Kor 9: 6-10;
Zab 112: 1-2, 5-9 (K) 5;
Yn 12: 24-26.

MBEGU YA IMANI!

Yesu Kristo leo anafundisha kwa kutumia mfano wa mbegu ambao tutaelewa kwa haraka zaidi. Kwakuwa ili mbegu iweze kumea ni lazima ibadilike kutoka kwenye hali yake ya mwanzo, ipokee hewa, maji, mwanga na mazingira ambayo itairuhusu kukuwa. Kama itajiruhusu yenyewe kubadilika, hapo tutaona mizizi ikichomoza, baadae majani, alafu matawi, na baadae kuwa mti nakutoa matunda au mbegu zinazofanana na mbegu ya mwanzo iliyokufa.

Katika historia ya Ukristo, tunaambiwa ni kwasababu ya damu ya mashahidi. Kanisa la mwanzo limekuwa na kumea katika hali hii hii kwa miaka elfu mbili iliyopita. Kwakifupi, “damu ya Mashahidi ni mbegu ya Kanisa.” Wafiadini (Mashahidi) ni wale waliouwawa kwasababu ya imani yao, na hiyo ilikuwa ni kulinda Imani yao ndani ya Yesu Kristo. Wote waliomwaga damu yao kama Mt. Laurent, wamekuwa kama mbegu iliokufa nakutoa matunda. Mashahidi walikufa wakijitahidi kutetea Imani yao ndani ya Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa njia ya vifo vyao, watu wengi wamekuja kumuamini Kristo. Leo, Yesu anatualika kujitolea maisha yetu ili kuungama Imani yetu ndani ya Kristo. Tunapaswa kuzuia yote yasio katika mpango wa Mungu, ili tuzae matunda mema na tuweze kupokea uzima wa milele na kuwa naye daima.

Sala: Bwana, nakuomba niwe mbegu ya Imani. Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni