Alhamisi. 28 Novemba. 2024

Tafakari

Alhamisi, Agosti 03, 2017

Alhamisi Agosti 3, 2017
Juma la 17 la Mwaka

Kut 40:16-21, 34-38
Zab 84: 2-5, 7, 10 (K)
Mt. 13:47-53


KUUTAFUTA UFALME

Leo Yesu katika somo la Injili anawambia wafuasi wake wachague njia ya hekima kwa kutumia mfano. Analinganisha ulimwengu kama bahari kubwa na watu ndani yake kama samaki. Kuhubiri Injili ni sawa na kurusha jarife katika bahari hii na kuvua vitu, kwa ajili ya utukufu. Wale wote waliotambua thamani yao katika Kristo wanachaguliwa kuishi naye milele. Wale wenye umakini, waaminifu katika injili, waandishi, wale waliowaaminifu katika Injili kushika maandiko na wale walio waaminifu katika kufundisha thamani za Injili. Yesu anamfananisha na mtu mwenye nyumba ambaye mambo yake ya zamani na utambuzi wake mpya vinamsaidia kutangaza lulu (Yesu) ambayo waandishi waliitambua. Yesu anatuambia kwamba yeye ni wa thamani kubwa. Atakaye mpata atakuwa na hekima na hatapotea kamwe na atakuwa kama huyu mwandishi mwenye hekima ambaye anatambua kutumia akili yake kwa utukufu wa Mungu.

Katika nyakati zetu “DHAMBI” inakubalika sana na inachukuliwa kuwa ‘kawaida tu’. Tamaduni zetu za ulimwengu zinaonekana kukuwa sana na kuchukulia kila kitu kuwa kawaida tu na kuhalalisha. Kuporomoka kwa maadili kunaonekana kuwa kawaida tu. Na katika hali hii kuna hatari kwetu kuona dhambi na kuiona kuwa ni kawaida tu na kuikubali. Tunapo itambua dhambi na kuitaja kwamba nidhambi na kuionesha daima Ulimwengu hutuchukia. Itakuwa ni utamaduni mbaya kama tukiifanya siku ya Mungu (jumapili) kuwa tamaduni nyingine tofauti na siku ya kumtukuza Mungu. Au pengine itakuwa ni utamaduni mbaya kubadili maadili ya ndoa. Sisi wenyewe tunaweza kutambua yapo mambo ambayo yapo kinyume na Imani yetu na ambayo yanavamia Imani yetu. Yesu yupo makini kuhusu dhambi na madhara yake. Anataka sisi tuishi kitakatifu na hivyo tuwasaidie wale wote walioshikwa katika dhambi na kuwasaidia wabadili maisha yao na kuyafanya yawe mapya.

Tafakari sana leo, juu ya nafsi yako mwenyewe ni kwa jinsi ghani unavyo ipinga dhambi. Dhambi ni mbaya na inaharibu maisha ya watu. Unapaswa kumpenda mtu aliye katika dhambi ili uweze kumsaidia kutoka huko, na wala usimtie moyo kubaki katika dhambi yake inayo pingana na mapenzi ya Mungu. Kusimama imara katika kupinga tamaduni mbaya zaweza kuwaokoa watu na kuwafanya wasiingie katika “kulia na kusaga meno” aliyosema Yesu. Je, wewe ni shahidi wa Injili, wa kuwatoa watu kwenye dhambi na kuwapeleka pwani ya Ufalme wa Mungu?

Sala: Bwana, pale dhambi ilipotufunga tumeshindwa kupata neema zako. Neema yako inahitajika sana katika ulimwengu wetu na katika maisha yangu. Nisaidie mimi niweze kusimama imara katika kupinga dhambi ili niweze kuwa kati ya wale watakaoshiriki katika ufalme wako. Nisaidie niweze kuwasaidia wote walio katika njia ya uharibifu. Yesu, nakuamini wewe. Amina

Maoni


Ingia utoe maoni