Jumanne, Agosti 01, 2017
Jumanne Agosti 1, 2017
Juma la 17 la Mwaka
Kumbukumbu ya Mtakatifu Alfonsi wa Liguori
Kut 33:7-11;34:5-9.28
Zab 103: 6-13 (k) 8
Mt 13:36-43
KUKUWA KATIKATI YA MAGUGU
Somo la Injili la leo linatualika kutafakari juu ya ufalme wa Mungu. Yesu alikuja kutangaza na kuanzisha Ufalme wa Mungu. Somo la kwanza linatangza na kutambulisha ukuu wa Mungu, ambaye ni mkarimu na mwenye huruma. Ingawaje yeye ni mkuu wa ulimwengu mzima na ni mkuu sana lakini anaongea na Musa kama vile rafiki anavyo ongea na rafikie. Anatupa uhuru wa kuijiingiza katika ufalme huu.
Katika mfano wa ngano na magugu, kila mmoja anapata neema wakati wa maisha yake, lakini wakati wa mavuno kila mmoja atahukumiwa kwa kadiri yake. Kati yetu tuna bahati ya kuzaliwa katika familia ya Kikristo. Mungu ametupa bahati ya ubatizo hata kabla hatujafahamu. Anaendelea kutupatia neema kwa njia ya kanisa. Lakini zawadi hii haina maana tutaingia tuu mbinguni moja kwa moja bila kujitahidi kuishi kadiri yake. Kati ya zawadi kubwa aliyotupa Mungu ni uhuru wa kuchagua mapenzi yake au kuyakataa. Tukitumia uhuru wetu vizuri tutatambua kama sisi ni magugu au ngano.
Jaribu, kufikiria kama Yesu angekuja kesho, na kutoa haki katika dunia yote, je utakuwa na wasi wasi kwasababu ya kukosea mtu haki? Pengine hapana. Lakini pengine tungefurahi kwamba haki inakuja. Mwisho wa ulimwengu kwa Mungu ni sawa kama utakavyo kuja wakati wake utakapo tokea. Mungu ni wazi yupo katika usukani wa ulimwengu. Anafahamu analolitenda na atakuwa na utukufu wa mwisho kwa kila kitu.
Wakristo wanaitwa kuwa chachu katika ulimwengu huu tunaoishi ili iweze kuwa sehemu nzuri ya kuishi. Kama sisi ni mashahidi wazuri, Injili itaenea vizuri sana kila mahali. Kuingia kwetu katika ufalme wa Mungu umejikita katika uchaguzi wetu wakuchagua kile kilicho chema na kukataa yote yanayo pingana na Mungu. Wito wetu kama wakristo ni kuwa mwanga na chumvi ya ulimwengu.Tunaomba hii iwe sala yetu kwa Mungu ili tuweze kufanywa upya ili roho nyingi ziweze kumpenda Mungu na kuwa raia wa mbinguni.
Sala: Bwana Yesu Kristo, ninatamani kukupa thamani ya kila kitu ya maisha yangu. Ninaomba niache yote ambayo ni kikwazo cha mimi kutokuja kwako, kukupenda na kukuabudi. Ninaomba nitafute Ufalme wa Mungu katika hali zote. Yesu nakuamini wewe. Amina
Maoni
Ingia utoe maoni