Jumapili, Julai 30, 2017
Jumapili, 30 Julai, 2017,
Juma la 17 la Mwaka
1 Fal 3: 5, 7-12;
Zab 118: 57, 72, 76-77, 127-128;
Rom 8: 28-30;
Mt 13: 44-52
YESU KRISTO, HAZINA YANGU
Mwaka 1936, Edward VI Mfalme wa England, alitokea kumpenda Valcin, msichana wa kawaida. Kadiri ya mapokeo, Mfalme alikuwa na uwezo tu wa kuoa kutoka katika familia tajiri. Alikuwa na chaguzi mbili tu. Amue kuacha ufalme wake na kumuoa Valcin au kumuacha Valcin na kubaki katika ufalme wake. Lakini wote wawili walikuwa na kitu kimoja, walikuwa watu wa ndoto.
Katika somo la kwanza tunamuona Mungu anamtokea Mfalme Sulemani na kumpa uchaguzi wa kufanya: “niombe kitu nami nitakupa”. Na wakati Sulemani alivyosema “nipe moyo wa kuelewa na hali ya kuweza kutofautisha mema na mabaya”, anaomba uelewa ili aweze kuwahudumia watu wake, aweze kutenda kwa huruma na pia aweze kutambua mema na mabaya. Sulemani anatambua vitu viwili (i) Hekima yote inatoka kwa Mungu (ii) kwa kuwa na hekima mambo yote yatakuja. Kwa kutumia lugha tunaweza kusema kwamba Sulemani aliomba “lulu” ya thamani kubwa. Na aliipata. Somo linatufunsdisha kwamba tunapo yatimiza mapenzi ya Mungu tunakuwa katika njia njema na katika mstari wa ufalme wake.
Na somo la Pili barua ya mtume Paulo inatupa mambo mawili (i) mambo yote ni mazuri kama tunatenda kwa upendo wa Mungu, tunaoitwa kwa mapenzi yake (ii) Na wote aliowaita aliwachagua na pia kuwahalalisha na pia kuwapa utukufu. Na sehemu muhimu ni kwamba Mungu anawaita watu kwa ngazi mbali mbali waweze kufurahia ufalme wake wa milele. Mungu ametuita kutuhalalisha na kutupa utukufu. Paulo anavyosema Mungu anawaita, hana maana kwamba anawaita baadhi kumtumikia na wengine kupotea. Mpango wa Mungu nikuwa wote waweze kukombolewa. Hii ina maana kwamba ni mapenzi kamili ya Mungu kwamba watu wote wakombolewe kuwaruhusu watu wakubali mapenzi yake au wakatae wenyewe kwa uhuru wao.
Katika somo la Injili Yesu anahitimisha safari ndefu ya mifano kuhusu ufalme wa Mungu kwa kuawasifu wake na waume wale wote waliokuwa werefu katika kumsikiliza na kumuelewa na kujikita katika ujumbe wake. Yesu anaendelea kufundisha kuhusu “Ufalme wa Mbinguni” kwa kutumia habari ndogo za Wagalilaya.
Yesu anatuambia kwamba Hekima ya kweli ni kutambua lulu ya thamani kubwa na kuuza vyote na kuinunua. Mifano yetu miwili katika somo la Injili, kuhusu, thamani iliofichwa na lulu-ni fundisho la kuachana na malimwengu na kujikita kwa Kristo kwa kufanya ufalme wake uweze kukuwa ulimwenguni katika hali ya kweli. Matayo mtoza ushuru huenda na yeye alitambua kitu kama hiki alivyo amua kuacha vyote na kumfuata Yesu wa Nazareth. Alivyo mtambua Yesu na hekima yake, mambo yote mengine yalikuwa ni ya ziada. Yesu pia anaweza kuja katika maisha yetu ya kila siku bila sisi kujitambua kama alivyokuja kwa Mathayo.
Mfano wa kuvua samaki kwa kutumia neti: katika Palestina kulikuwa na njia mbili za kuvua samaki, wa kwanza ilikuwa kurusha neti, katika hali ya akili kubwa na utalaamu mkubwa pia kwa wakati. Aina ya pili ilikuwa ni kulazi neti chini. Na baada ya kushika, kulikuwa na kuokota baadhi na mengine kutupa, samaki wazuri walipelekwa sokoni na wengine wabaya kutupwa. Na kama neti hii ya kulaza chini inavyo kusanya samaki wazuri na wabaya, kanisa pia lina watu wema na wabaya, watakatifu na wadhambi. Kama ilivyokuwa kwa ngano na magugu, mfano huu unatuonya na hali ya kuhukumu kabla, lakini pia inatuonya kuhusu hukumu inakayo kuja.
Kuwa Mkristo Mkristo ni sawa na kuwa kama mtu anaye itafuta lulu. Kuwa mkristo ni sawa na kuwa mtu anayewinda lulu. Inagharimu majitoleo makubwa na sadaka. Lakini pia kuna tofauti kubwa kati ya wakristo na wengine. Paulo anaonesha kwa barua yake kwa Wakorintho “wachezaji wanafanya mazoezi katika hali zote, wanafanya hivyo ili kupata lulu inayo haribika, lakini sisi tunafanya hivyo ili kupata lulu isiyo haribika” (1 Kor 9:25) hali hii ni tofauti. Lulu tunayo tafuta kama Wakristo ni lulu ya thamani isiyo haribika.
Ndio maana Injili ya leo inatoa ujumbe huu muhimu. Hakuna kitu chochote ulimwenguni kinachoweza kuchukuwa nafasi ya Mungu. Inatuambia pia kilicho na maana zaidi tutakapo kufa ni maisha tutakayo ishi, jinsi tutakavyokuwa. Mifano hii inataka kutuambia kwamba wakati mmoja anapo mgundua Yesu katika maisha, vingine vyote vinakuwa ni ziada. Na hiki ndicho Mt. Paulo anacho maanisha anavyosema “kuishi kwangu ni Kristo na ufa ni faida” (Fil 2:21). Kuwa na uhusiano binafsi na Yesu na pia na wengine wengine kumfanya Yesu kuwa ndio kioo cha maisha yao-ni kitu muhimu sana ulimwenguni humu. Yesu anavyo onekana katika maumbo ya mkate na divai, tumpe nafasi ya kwanza na ya hali ya juu.
Sala: Bwana Yesu Kristo, ninatamani kukupa thamani ya kila kitu ya maisha yangu. Ninaomba niache yote ambayo ni kikwazo cha mimi kutokuja kwako, kukupenda na kukuabudi. Ninaomba nitafute Ufalme wa Mungu katika hali zote. Yesu nakuamini wewe. Amina
Maoni
Ingia utoe maoni