Alhamisi. 28 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatatu, Julai 24, 2017

Jumatatu, 24 Julai 2017
Juma la 16 la Mwaka

Kut 14:5-18
Kut 15:1-6 (K)1;
Mt 12:38-42


MKUBWA KULIKO YONA!

Kuna watu kati yetu ambao hawajawahi kuwa na furaha, haijalisha unajitoa mara ngapi kwa ajili yao, daima hawana furaha na wanalalamika daima. Licha ya mambo makuu ambayo Mungu ametenda katika maisha yao, hawajawahi kuridhika. Wayahudi daima walitarajia muujiza kutoka kwa nabii ili waweze kudhihirisha kama ni nabii wa kweli. Hawakumuamini Yesu na wanaulizia ishara nyingi na miujiza ili waweze kumwamini. Lakini hata kama Yesu angetenda muujiza mwingine wala isingeleta mabadiliko. Kwasababu alivyo mponya yule kijana ambaye alikuwa kipofo (Mt12:22) walimshtumu kwa kutenda miujiza kwa kutumia nguvu za Belzebul, mkuu wa pepo.

Yona alikuwa ishara. Alikaa muda wa siku tatu ndani ya tumbo la nyangumi. Ni wazi kwamba walifahamu kwamba amekufa. Lakini nyangumi alitumika kama chombo cha Mungu ili Yona aweze kwenda Ninawi kwenda kuhubiri toba. Na kweli walitubu na kubadilisha maisha yao. Giza ndani ya tumbo la nyangumi mwishoni, inabadilika na kuwa Baraka na ishara kwa miaka iliyokuja. Habari ya Yona ilitoa ishara ya kifo cha Yesu, siku tatu ndani ya kaburi na kufufuka kwake. Hii ndio ishara ambayo Yesu alikuwa aitoe na anaendelea kuitoa. Ni ishara ya matumaini makubwa tukiichukulia vizuri.

Lakini mara nyingi tunaweza kuanguka katika majaribu makubwa. Ni mara nyingi pia tunataka ishara zaidi ya ishara ambazo Yesu ameshatupatia. Tunataka uhakika mwingine kutoka kwa Mungu kuhusu mapenzi yake. Tunataka yeye aongee kwa ufasaha na kwa sauti. Yesu yupo nasi daima katika Ekaristi takatifu, akituponya kutoka katika magonjwa yetu. Yesu Kristo yupo ndani ya jirani zetu tunaokutana nao. Ishara kuu ni Mungu kuwa Mwanadamu na Neno kutwa mwili kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.

Yesu anatukumbusha sisi kwamba tunapaswa kuamini kila kitu alicho ongea, hata kama tunajisikia tupo katika giza kuu kama lile la tumbo la samaki au ndani ya kaburi, matumaini hayajapotea. Mungu yupo katika vitu vyote na yupo kati yetu hata pale ambapo tunaona yupo kimya. Anaongea nawe muda wote. Jifunze kuchagua mapenzi ya sauti yake.

Sala: Bwana, naomba unisaidie kukuamini wewe daima hata kama sioni miujiza na ishara kutoka mbinguni. Nisaidie kukuamini hata katika wasi wasi na mashaka na udhaifu wangu katika maisha. Ninaomba unipe Imani kamili katika kujibu wito wako katika maisha yangu. Yesu anakuamini wewe. Amina

Maoni


Ingia utoe maoni