Alhamisi. 28 Novemba. 2024

Tafakari

Jumapili, Julai 23, 2017

Jumapili, Julai 23, 2017,
Juma la 16 la Mwaka

Hek 12:13, 16-19
Zab 85:5-6,15-16;
Rom 8:26-27
Mt 13:24-43


SHUHUDA WA UPENDO WA MUNGU ULIMWENGUNI

Ulimwengu ulikuja kutoka katika uzuri mikononi mwa Mungu. Uumbaji ulianza kwa kugawa mwanga na giza(Mwa 1:4). Mungu alisema na “kuweko Mwanga katika anga kugawa usiku na mchana” (Mwa 1:14). “Mungu aliona yote aliyokuwa ameumba na tazama ilikuwa nzuri sana” (Mwa 1:31). Lakini tangia hapo mwanadamu alivyo anza, bila kujua, kuogopa utofauti imeanza kuleta mchanganyo. Alianza kutenga kati ya uzuri na ubaya, kilicho safi na kisicho safi, kitakatifu na kisicho kitakatifu. Uwepo wa ubaya ulimwenguni umebaki kuwa usumbufu kwa mwanadamu. Hakubali ukweli katika ulimwengu sehemu ambayo uzuri na ubaya upo.

Katika somo la leo kutoka katika kitabu cha Hekima, mwandishi anaandika kuhusu “Haki ya Mungu. Mungu hatumii nguvu zake kutuadhibu. Anatumia tu kwa ajili ya uzuri wa Mwanadamu. Hii ndiyo haki; kutumia hekima kwa wote. Ukuu wake ni wa mahali pote, hufunika walio wema na wabaya pia. Hawapendi tu baadhi bali anawapenda wote. Wakati watu wanatumia nguvu kuogopesha wengine na kuweka hofu kwa watu au kujiweka katika hali ya kukandamiza wengine na kuwa katika hali ya juu. Mungu pamoja na kwamba yeye mwenyewe ndiye chanzo cha nguvu yote, hatumii kutisha watu wala kutumia kuadhibu, au kurudisha kisasi, bali hata katika yote yeye huonyesha huruma kwa walio dhaifu kwa ukarimu.

Katika somo la Pili Paulo anakiri kwamba sisi hatufahamu kusali. Roho ndiye anaye tusaidia kusali na kutufundisha ni maneno ghani tutumie tuweze kupeleka maneno yetu kwa Baba. Kusali kwa Mungu ni kufungua akili na mioyo yetu kwake na kuwa tayari kupokea mapenzi yake katika maisha yetu. Sala inayotokana na Roho daima inajibiwa kwasababu inakuwa inalingana na mapenzi ya Baba. Haijaribu kujitafutia mambo yake bali inatubadilisha na kutuunganisha na mapenzi ya Mungu.

Katika somo la Injili ndani ya mifano mitatu, Yesu anatufumbulia mafumbo ya ufalme wa Mungu. Je, magugu yanatoka wapi? Chanzo cha na uwepo wa uovu unahitaji maelezo. Mathayo anayatoa kwa mfano wa Yesu. Kwanza kabisa ni mwenye shamba. Huyu anamwakilisha Mungu, yeye ambaye ndiye anaye sia mbegu na kuangalia ubora wa mbegu. Wa pili ni adui,anaye wakilishwa na kinacho onekana bora katika ulimwengu. Huyu anakuja usiku na kusia magugu ambayo yanaonekana kuwa kama ngano. Mizizi yake imesongana na ngano kiasi kwamba ni vigumu kuiondoa bila kuiondoa na ngano pia. Mhusika wa pili ni mtumishi ana mwakilisha kila mmoja wetu. Wanavyo fanya ni kama sisi tunavyo kumbana na uovu ulimwenguni, katika jumuiya zetu, au kwa kila mtu. Wanaonesha kujitoa kwao katika shamba kwa ajili ya uzalishaji. Wanakosa subira, wanavutwa na tamaa ya kutaka kuyaondoa magugu mara moja. Lakini mwenye shamba yeye ni mpole. Wala hashangazwi na hali hii. Subira ya Mungu ni kubwa na anawaambia waache magugu na ngano ziote pamoja. Katika ulimwengu huu uzuri na uovu havitengani. Vipo vitaota pamoja mpaka mwisho. Mpango wa Mungu pia anataka tutambue ulimwenguni kuna uzuri na ubaya na kwamba vipo na vinaishi ulimwenguni, na hivyo tunapaswa kupokea katika hali ya maisha yetu. Uwepo wa magugu ndani mwetu unataka kutuambia pia kwamba “Hakuna mwenye haki duniani anaye tenda mema tu na ambaye hatendi dhambi” (Ybs :20). Hapa si kuhalalisha uovu, bali Yesu anataka tufahamu hilo na kwenda katika hali ya uvumilivu tukiwa na macho ya Kimungu.

Baada ya mfano huo unafuatwa na mifano mingine miwili pacha. Inaitwa mifano pacha kwasababu huleta ujumbe sawa: kwamba kulinganisha kile cha kwanza ambacho kilikuwa kidogo sana na matokeo makubwa. Mbegu ya haradali ambayo ni ndogo sana ambayo ni vigumu kuona kwa macho hukuwa na kutoa matawi makubwa, na chachu kidogo huchachusha unga wote. Ulinganishaji wake wa pekee. Mifano hii ni mwaliko wa kumtumainia Mungu.

Mifano hii ni ni mifano yetu sisi katika Jumuiya za Kikristo. Mbegu sio akili ya ulimwengu huu bali Mwana wa Mungu, Yesu. Pengine wakristo wa kwanza walipumzika mno hawakuchukulia kwa makini ahadi zao za ubatizo. Mathayo katika kuwamsha anawatikisa na kuwakumbusha kuchukulia maisha katika uhalisia. Hakufanya hivyo kuonesha kwamba ni nini kitatokea kwa wadhambi bali alitaka kuwaamsha wakristo. “Hakumtuma Mwanae ulimwenguni ili kuhukumu ulimwengu bali ulimwengu uokolewe kwa njia yake” (Yn 3:17). Je, vipi kuhusu moto? Mungu anautambua moto mmoja : Roho wa Mungu ambaye alishuka siku ya Pentekoste (Mdo 2:3). “nimekuja kuwasha moto ulimwenguni ni kwa jinsi ghani ninatamani kama umekwisha waka’? (Lk 12:49). Ni moto usiozimika utakao choma magugu yote ndani ya mioyo ya kila mmoja wetu, na kuacha tu ngano safi ambayo inahitajika katika ulimwengu ujao. Sio tangazo la kutishia na kuadhibu bali ni tangazo la kwamba siku moja Roho wa Mungu atasafisha maovu yote. Katika Ufalme wa Mungu hakutakuwa na mmoja atakayefanya kinyume.

Na mfano wa pili wa mbegu ya haradali unataka kutueleza kwamba hakuna mtu mdogo sana au mdhambi sana anayetengwa na Ufalme wa Mungu. Na pia hakuna mtu mkubwa sana anayeweza kujidai kuwa na haki zote za ufalme wa Mungu. Mungu anaweza kuvuna mavuno mengi kutoka katika moyo uliokuwa umepondeka. Mmoja anavyo jinyenyekesha kwa Bwana, na kumchagua yeye katika mambo yote, matunda huwa mengi ajabu.

Mfano wa tatu kuhusu chachu, huleta ukweli huu. Wengi wetu tunaweza kujifirikia sisi wenyewe kwamba ni wadogo sana kiasi ambacho hatuwezi kuleta mabadiliko yeyote katika jamii zetu. Chachu huwekwa katika hali ya udogo sana lakini huchachusha unga wote. Wakristo tunaitwa kuwa chachu ili tuweze kufanya ulimwengu huu sehemu nzuri ya kuishi. Kama sisi ni mashuhuda wazuri wa Injili, Neno la Mungu litaenea kila mahali. Kazi yetu kama Wakristo ulimwenguni ni muhumu sana . Tunaitwa kuwa chumvi na mwanga katika Ulimwengu huu. Kuwa ngano kati ya magugu. Kuwa kama mbegu ya haradali inayokuwa na kuleta sehemu ya kupumzika na kupata makao kwa watu, kuwa mashahidi wa upendo wa Mungu ulimwenguni. Tunaomba hali hii iweze kuwa sala yetu ya kila siku kwa Bwana, ili tuweze kubadilishwa na kuleta mabadiliko, ili Roho nyingi ziweze kupata wokovu na kufahamu upendo wa Mungu na kuwa raia wa ufalme wa Mungu.

Sala: Bwana, mimi ni mdhambi, na wewe mwenyewe ni Mtakatifu. Nipe nguvu zako na neema ili niweze kuishi maisha kadiri ya mapenzi yako. Ninaomba nisimame kwa ujasiri katikati ya uongo na uovu ambao unanizunguka. Ninaomba nikaze macho yangu daima kwako, wewe ambaye ni Mchungaji mkuu. Ninaomba niwe shahidi wa upendo wako katika familia, jirani zangu na Kanisa. Yesu, ninakuamini wewe. Amina

Maoni


Ingia utoe maoni