Alhamisi, Julai 06, 2017
Alhamisi, Julai 6, 2017.
Juma la 13 la Mwaka
Kumbukumbu ya Hiari ya Mt. Maria Goreti
Mwa 22: 1-19;
Zab 115: 1-9;
Mt 9: 1-8
UJASIRI WAKUTAFUTA MSAMAHA
Somo la Injili linamalizia kwa Yesu akimponya mtu aliye pooza na kumwambia “achukue mkeka wake na kwenda nyumbani”. Huyu mtu alifanya hivyo na hapo watu wakashangazwa. Kuna miujiza miwili inayotokea hapa. Wa kwanza ni muujiza wa kimwili na mwingine muujiza wa kiroho. Muujiza wa kiroho ni kwamba huyu mtu alisamehewa dhambi zake. Muujiza wa kimwili ni kupona kutokana na kupooza kwake. Unadhani ni muujiza ghani huyu mtu alihitaji zaidi? Ni muujiza ghani kati ha hizi ulikuwa ni muhimu? Ni vigumu kujibu swali la pili kwasababu hatujui mawazo ya huyu mtu yalikuwaje, lakini swali la kwanza ni rahisi. Uponyaji wa kiroho, msamaha wa dhambi, ni muhimu zaidi sana kuliko kati ya hii miujiza miwili. Ilikuwa ni wa muhimu sana kwani una umuhimu katika maisha ya umilele ya roho yake.
Sisi mara nyingi ni rahisi kusali kwa Mungu kwa ajili ya mahitaji ya kimwili au mengine. Tunajisikia rahisi kumuomba Mungu baraka hizo. Lakini ni rahisi mara ngapi kwetu sisi kuomba msamaha? Hili linaweza kuwa ngumu sana kwa mtu kufanya kwasababu inahitaji unyenyekevu wa ndani kutoka upande mmoja. Inatuhitaji kukubali kwamba sisi ni wakosefu tunao hitaji msamaha. Kukubali kwamba nahitaji msamaha inahitaji ujasiri, lakini ujasiri ni fadhila na inafunua nguvu kubwa ya tabia upande wetu. Kuja mbele ya Yesu na kuomba huruma yake ni kitu kikubwa ambacho twaweza kufanya na ni msingi wa sala yeyote tunayo fanya mbele yake. Tujiulize una ujasiri kiasi ghani katika kujinyenyekesha mbele ya Mungu na kuomba msamaha, na kukubali kwamba wewe ni mdhambi.
Sala: Bwana, nipe ujasiri. Nipe ujasiri hasa katika kujinyenyekesha mbele yako na kukiri dhambi zangu. Kwa kukubali huku kwa unyenyekevu, nisaidie mimi niweze kutafuta huruma na msamaha wako kila siku katika maisha yangu. Yesu, nakuamini wewe.Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni