Alhamisi. 16 Mei. 2024

Tafakari

Jumapili, Julai 02, 2017

Jumapili, Juni 2, 2017.
Dominika ya 13 ya Mwaka

2 Fal 4: 8-11, 13-16;
Zab 88: 2-3, 16-19;
Rom 6: 3-4, 8-11;
Mt 10: 37-42.


NYUMBA MPYA, FAMILIA MPYA

Neno nyumba katika lugha ya Kiebrania haina maana tu ya jengo bali pia familia. Mtu hawezi kufanya lolote tofauti na maana hii: “kwa wengine ni vitu ambavyo huwezi kuishi bila hivyo: maji, chakula, nguo na nyumba kwa ajili ya makazi” (YbS 29:21). Lakini yule ambaya anataka kuanzisha familia mpya, anapaswa kuacha nyumba yake: “Mwanaume atamuacha Baba yake na mama yake na ataungana na mkewe na wote wawili takuwa mwili mmoja” (Mwa 2:24). Ni kitendo cha kuacha nyumba moja na kuingia katika nyumba nyingine au familia mpya. Yesu pia ana uacha mji wake mwenyewe Nazarethi, “Mwana wa mtu hana mahali pa kulaza kichwa chake” (Mt 8:20). Aliacha familia yake: ‘Mama yangu ni nani’? ‘Kaka zangu ni akina nani?’ na kwenda katika familia mpya ‘tazama! Wapo hapa mama yangu na kaka zangu (rejea. Mt 12:48-50). Kwa wale wote wanaopenda kumfuata Yesu, anawaambia wachukue jukumu hilo hilo: ujasiri wakujitenga, kuchukua hatua kubwa kuelekea katika ukweli halisi, kutambulishwa katika nyumba mpya, familia mpya, familia ya wana wa Mungu.

Katika somo la kwanza tunamuona nabii Elisha akibariki wana ndoa wawili, waliokuwa wana umri mkubwa bila kuwa na watoto, na hivyo anawahidia mtoto. Kwa kujua kwamba Elisha ametokea katika nchi ya mbali na hakuwa na nyumba wala familia alimkaribisha na kumshirikisha. Huyu mwanamke ambaye alikuwa tajiri, alikuwa na uwezo wa kumpatia Elisha fedha kidogo na kumwacha aondoke, lakini hakumpa tu msaada bali alimkaribisha pia nyumbani kwao, na kumkaribisha na kujisikia kama mmoja wao katika familia. Ishara anazofanya huyu mwanamke zina mfurahisha Mungu, na hivyo Mungu anampa furaha kubwa ambayo alikuwa akiitamani: alimpa mtoto wa kiume. Elisha ana wakilisha mitume, ambao hata leo, wana acha nyumba zao, nchi yao, familia zao na kujitoa kwa ajili ya kazi ya Mungu na Injili.

Katika somo la pili, tunaona kwamba Ubatizo ulikuwa ni utamaduni uliokuwepo kipindi cha Yesu. Wale wote walioufuata walibatizwa. Ilikuwa ni ishara iliyo fanya mabadiliko makubwa katika maisha: kifo kwa mambo ya zamani na kuzaliwa upya. Hata ubatizo wa Kikristo una maana hiyo hiyo. Maji ya ubatizo yalichukuliwa kama maji tumboni mwa mama ambamo mtoto mdogo huishi katika mazingira hayo na baadaye huzaliwa kama mtoto wa Mungu. Paulo anasema “kwa njia ya ubatizo, tunazikwa pamoja na Kristo ili tufufuke naye katika maisha mapya” . kama ubatizo ni ishara ya kuzaliwa upya, ina dhihirisha mwanzo wa maisha yote ya maaldili mapya, mkristo hawezi kuendelea kutenda vitu vya zamani, anapaswa kuchukulia yeye mwenye kama mfu katika dhambi, na mzima na anayeishi kwa Mungu ndani ya Kristo”.

Katika Injili, Mathayo anaendeleza na utume wa wanafunzi wa Yesu. Kwanza kabisa, wito wa Yesu kuhusu ufuasi umeonesha katika hali yote. Kuacha na kukataa yote inahitajika katika maisha ya ufuasi. Kila agizo linafuatiwa na ugumu na hali ya kweli ya kuacha yote. Zaidi ya yote, Yesu anataka wafuasi wake kuondoka katika hali za ndani za hisia zao, kama vile kuwapenda wazazi au watoto.

Yesu hafanyi hivi kutaka kukataa sheria ya Musa (Torati), inayo amuru kuwa heshimu Baba na Mama. Ni hakika kwamba, ameirudia amri kwa msisitizo (Mt 15:4). Matayo ameandika Injili yake kipindi cha madhulumu. Wafuasi walikuwa wameshapatwa na magumu ya kubaki waaminifu kwa Kristo, walipaswa kuvunja vifungo ambavyo walikuwa wamejifungia na watu muhimu tu kwao. Marabi walikuwa wamesha amua kuwatenga wafuasi watakao amua kumfuata Yesu, na kuwatenga na sinagogi, na kuwaona kama wazushi, na wala familia zao wasiwatii. Yesu aliwaamuru wafuasi wake wawe na ujasiri wa kusimama imara hata kama hawana wa kuwaunga mkono, kuwalinda, na hata bila mali kwa ajili ya Injili. Na pia aliendelea na ombi lingine, tena lenye maana kubwa zaidi: kuwa tayari kuyatoa maisha yao.

Ishara ya msalaba ni ishara ambayo haikwepeki kwa mfuasi yeyote anayependa kumfuata Kristo na kuishi matakwa ya Injili: kama Bwana wao, watakutana na msalaba, nao ni machungu ya ulimwengu. Hata kama maisha hayataondolewa kwa njia ya kuuwawa, wanapaswa kutoa kuyatoa maisha yao kwa ukarimu na kama sadaka kwa ajili ya watu.

Katika upande wa pili wa Injili, ni zawadi kwa wale wote watakao wakaribisha wale wanao ihubiri Injili, “Kila anaye wakaribisha ninyi, ana nikaribisha mimi” (mstari. 40). Hii ni kama ule ukaribisho aliopokea Elisha katika somo la kwanza. Kila anaye mkaribisha nabii kwasababu ni nabii, atapokea zawadi ya kinabii. Hata upendo kidogo ukao tolewa kama vile kumpatia mfuasi kikombe kidogo cha maji ya baridi, ingawaje ni kidogo, hakika hakita sahaulika.

Kwa hiyo kila mfuasi anaitwa kuwasaidia wale wote waliojitoa kwa ajili ya kutangaza neno la Mungu. Kila Mkristo ana alikwa kuwakaribisha katika familia zao, watu kama hao, walio acha, nyumba, wake, waume, watoto kwa ajili ya kuwa na muda wote na Kristo na watu wake.

Tafakari leo ni kwa jinsi gani wewe ni sehemu ya familia ya Mungu. Tafakari kama unatamani kuwakaribisha nyumbani kwako hao wafuasi kama vile mapadre, watawa, na waamini, ambao kwa moyo usio gawanyika wameyatoa maisha yao kwa ajili ya kazi ya Bwana, kwa ajili ya kuwa tayari kwa ajili ya maisha yako ya kiroho. Viongozi wa dunia tafakari kama unampa Yesu nafasi ya kwanza katika maisha yako. Tujiunge pamoja ili kujenga familia ya Kristo.

Sala: Bwana, ninakupa maisha yangu yote kwako akili, moyo, utashi na nguvu. Nisaidie nikupende wewe zaidi ya yote na katika yote, na katika mapendo hayo nisaidie mimi niweze kuwapenda wale wote uliowaweka katika maisha yangu. Amina

Maoni


Ingia utoe maoni