Alhamisi. 16 Mei. 2024

Tafakari

Jumatano, Juni 28, 2017

Jumatano, Juni 28, 2017.
Juma la 12 la Mwaka wa Kanisa

Kumbukumbu ya Mt. Ireneo, Askofu na Mfiadini

Mwa 15: 1-12, 17-18;
Zab 105: 1-4, 6-9;
Mt 7: 15-20


HUKUNA MTI MZURI UNAO ZAA MATUNDA MABAYA!

Yesu alisema “utautambua mti kwa matunda yake.” Alitambua kuwa mti mzuri unazaa matunda mazuri na mti mbaya unazaa matunda mabaya. Wakati tunanunua matunda sokoni hasa machungwa kutaka kutambua kweli kama ni mazuri ni pale unapo onja moja, na sio kwa kutazama tuu rangi yake kwa macho. Wakati mwingine tunajishughulisha na jinsi tutakovyo onekana mbele za watu kwa kuvaa vizuri na kuwa safi, hii ni sawa lakini ukweli ni kwamba utendaji wa mtu ndio ukweli wa jinsi ya mtu alivyo sio mavazi. Tunaweza kuwadanganya wengi kwa muonekano wetu wa nje, lakini kudanganya huku huwa hakudumu kwa muda mrefu. Leo Yesu anatualika tujiulize: hivi mimi ninatoa matunda gani? Na anatuambia matunda yetu yanaweza kuwa mazuri tuu kwa njia ya maisha ya sala (kokomaa), sadaka (kupruni) na kuto fungamana na dhambi (kuweka dawa) na mali au malimwengu.

Mtu muovu hawezi kuzaa matunda mazuri. Ni vizuri kuwa na uelewa na ukweli kwamba “manabii wa uongo wapo”. Baadhi wana wapotosha wengine wazi wazi huku wakijionesha wanawatendea kitu kizuri, wengine wanatenda kama vile mbwa mwitu amevaa ngozi ya kondoo akiwa katikati ya kondoo, wakiwa na lengo la kupata mambo yao. Mtu anaye muuzia mtu gari alilo lipaka rangi vizuri huku akijua sio zuri, lakini akisifia kwamba ni gari zuri sana, lengo lake ni kuuza tu gari na kupata faida bila kujali madhara yanayoweza kusababishwa na gari hilo kwa anaye nunua.

Wakati ikifikia ni wakati wa kufanya mangamuzi, ufunguo ambao Yesu anatupa ni kuangalia matunda ambayo mtu anazalisha kwa kusema kwake au kutenda kwake. Kama kweli utaona uzuri kwa matokeo ya mangamuzi fulani, tambua kwamba hii ni alama zuri na imetoka kwa Bwana. Kama utaona matokeo mabaya kwa sababu ya mangamuzi fulani, yakileta matunda mabaya, ni alama zuri kwamba maamuzi unayo yatafakari hayajatoka kwa Mungu. Chagua matunda mazuri na utakuwa unachagua mapenzi ya Mungu.

Sala: Bwana, nipe neema ya kuchagua mapenzi yako katika maisha yangu daima. Nisaidie niweze kuona matunda mazuri ambayo yanakuja kwasababu ya kukufuata wewe daima. Ukiwa unazaa matunda mazuri katika maisha yangu, Bwana wangu, nisaidie niweze kutembea katika njia hiyo ya utakatifu yenye zawadi nyingi za matunda mema. Yesu, nakuamini wewe. Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni