Alhamisi. 19 Septemba. 2024

Tafakari

Ijumaa, Agosti 05, 2016

Ijumaa, Agosti 5, 2016,
Juma la 18 la Mwaka

Nah 2:1, 3:1-3, 6-7;
Kumb 32:35, 39, 41;
Mt 16:24-28


KUPOTEZA MAISHA YA NAFSI ILI KUPATA YOTE!

Yesu anatuambia katika Injili kwamba, ni lazima kujikana nafsi ili kumfuata. Kujikana maana yake ni, kutokujibakiza, kutokujijengea heshima, kukataa, kujiachia, kujiweka huru kutoka mambo ya vionjo binafsi. Ni kusema “Ndio” kwa Kristo na kusema “Hapana” kwa nafsi. Sababu ya kujikana ni kwamba mioyo yetu ni muhimu zaidi kuliko ulimwengu mzima. Mwanadamu akishapoteza roho yake, imepotea haiwezi kununuliwa popote nakurudishwa. Mwanadamu atakaye ipoteza, ameipoteza milele. Msalaba unaonekana katika hali ya kawaida kama mateso na kupoteza, lakini kwa kweli ni faida. Sadaka ya Kristo Msalabani imekuwa fidia kubwa kwetu na kuleta wokovu. Je nipo tayari kujikana mwenyewe, kuchukua msalaba wangu na kumfuata Kristo?

Sala: Mungu wangu, Mungu wangu, chukua yote kwangu yanayoniweka mbali nawe, Mungu wangu, Mungu wangu, nipe yote yanayo nileta karibu nawe, Mungu wangu, Mungu wangu, chukua ubinafsi ndani yangu na unipe yote katika wewe. Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni