Jumatano. 15 Mei. 2024

Tafakari

Ijumaa, Juni 23, 2017

Ijumaa, Juni 23, 2017,
Juma la 11 la Mwaka wa Kanisa

Sherehe ya Moyo Mtakatifu wa Yesu

Kumb 7: 6-11;
Zab 103: 1-4;
1 Yn 4: 7-16;
Mt 11: 25-30


MOYO UNAO WAKA MAPENDO!

“Huu ni upendo si kwamba sisi tulimpenda Mungu kwanza bali yeye alitupenda sisi kwanza akamtuma mwanaye ulimwenguni kama sadaka kwaajili ya dhambi zetu” (1 Yn 4: 10). Sherehe ya Moyo Mtakatifu wa Yesu ni sherehe ya upendo wa ukombozi wa Mungu wetu. Mungu anayetupenda alimtoa mwanaye aje ulimwenguni kama sadaka kwaajili ya ukombozi wa Ulimwengu. Upendo huu unaoneshwa katika moyo wa mwana wa Mungu. Neno “moyo” linasimama kama upendo wa mtu. Na hivyo watu husema “Nakupenda kwa moyo wangu wote” na wakati tunapo sheherekea sikukuu ya Moyo Mtakatifu wa Yesu kanisa linatuhimiza kutafakari juu ya upendo wa Mungu, upendo uliofunuliwa ndani ya mwili wa Mwanaye Yesu Kristo.

Ni Mungu aliyewachagua wa Israeli kuwa watu wake. Aliwabariki na akawachagua kuwa watu wake kati ya mataifa mengi. Si kwasababu walikuwa na nguvu kuliko wengine lakini kwasababu ya upendo wake. Hili ndilo Musa alilowafundisha watu wa Israeli. Anawakumbusha juu ya upendo wa Mungu juu yao. Upendo wa Mungu kwa watu wake hauna mwisho na hauna masharti. Aliwapenda watu wake pamoja na mapungufu yao na makosa yao. Na hata hivyo ubinadamu uliponaswa na dhambi alimtoa mwanaye wa pekee kwajili yetu. Kwahiyo tunapaswa kuuzoea nakuupenda upendo huu ili tuweze kuuelewa zaidi na kuwa watu wakweli wanotamani kuwa na Mungu daima. Ili tuweze kumpenda kwa moyo wetu wote na akili yetu zote.

Kwahiyo katika sikuu hii ya moyo Mtakatifu wa Yesu, tunamshukuru Mungu kwa upendo wake mkubwa kwetu anaotuonesha kila siku. Tuupende na kuushi upendo huu ndani mwetu ili tuweze kuwashirikisha na wengine.

SALA: Moyo Mtakatifu wa Yesu, utuhurumie. Ninakushukuru Bwana wangu kwa kunipa yote hayo. Hakuficha kitu kwangu na unaendelea kunigawia maisha yako kwa ajili yangu na kwa ajili ya ulimwengu mzima. Ninaomba nipokee yote unayonipa bila kubakiza chochote kutoka kwako. Yesu, nakuamini wewe. Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni