Alhamisi. 16 Mei. 2024

Tafakari

Jumamosi, Juni 17, 2017

Jumamosi, Juni 17, 2017.
Juma la 10 la Mwaka

Jumamosi kumbukumbu ya Bikira Maria.

2 Kr 5: 14-21;
Zab 103: 1-4, 9-12;
Mt 5: 33-37.


BWANA WAKO NI NANI?

Injili ya leo inatupa maada mbili zenye umuhimu: uhusiano wetu na fedha (Mt 6: 24) na uhusiano wetu na Neema za Mungu (Mt 6: 25-34). Ni kitu ghani kilichopo kati ya kutumikia ‘mabwana wawili’ na ‘tamaa’? Vina chanzo kimoja cha matatizo-kugawanyika ndani yake. Kiini cha neno tamaa, tunaweza kusema moja kwa moja kuwa ni “kuwa wa mitazamo miwili. Mtu wa tamaa mbili ni mtu wa kwenda na kurudi na huishia kushindwa kufanya uamuzi. Woga wa matokeo mabaya ni vitu vinavyo dumaza wale weye tamaa. Ni hali hiyo hiyo pia wale wanaopenda kumfuata Mungu na wakati huo maisha ya ulimwengu yanamvutia na anataka kujikita huko na kufanikiwa sana.

Ni nani aliye Bwana wa Maisha yetu? “Bwana’ wetu ni kile kinacholinda maisha yetu na mawazo yetu ya maisha, kutengeneza mienendo yetu, kuelekeza na kuhimili tamaa za moyo na thamani ya maisha tunayo chagua kuyaishi. Tunaweza kuongozwa na vitu mbali mbali-kupenda pesa au mali, madaraka na nguvu, kupenda utajiri na anasa, kuendeshwa na tamaa na kutekwa kiakili. Tuna Bwana mmoja ambaye anaweza kutuweka huru kutoka katika utumwa wa dhambi na woga. Bwana huyo ni Bwana Yesu Kristo.

Yesu anatumia mfano kutoka katika hali ya asili yetu kuonesha kwamba Mungu ndiye anaye tutegemeza. Katika sala ya Baba yetu tunakumbushwa kwamba Mungu ndiye anaye tutunza na kutulisha tunaposali: “utupe leo mkate wetu wa kila siku.” Mkate ni nini, ni kila kitu tunacho hitaji katika maisha kinacho tufanya tukuwe na kuishi. Tamaa mbaya haisaidii wala sio muhimu. Inaondoa ujasiri wetu na Imani yetu na kunyonya nguvu yetu ya kutenda mema. Yesu anawaonya wafuasi wake dhidi ya tamaa mbaya na uroho wa mali na badala yake watafute vitu vya Mungu-Ufalme wake na haki yake.

Sala: Bwana, nisaidie mimi niweze kuwa mtu ambaye BWANA wake ni wewe. Kwa wakati ambao nimerudi nyuma kwa kupenda mno fedha na mali kwa tamaa mbaya. Nisamehe. Nisaidie mimi daima niweze kufuata mapenzi yako matakatifu na kila wakati niweze kuacha njia ya upotofu. Yesu nakuamini wewe. Amina

Maoni


Ingia utoe maoni