Jumatano. 15 Mei. 2024

Tafakari

Ijumaa, Juni 16, 2017

Ijumaa, Juni 16, 2017,
Juma la 10 la Mwaka

2 Kor 4: 7-15;
Zab 116: 10-11, 15-18;
Mt 5: 27-32


KUINGOA DHAMBI KUTOKA KATIKA MAISHA YETU!

Tukiangalia katika somo la Injili ya leo tunaweza kushangazwa na maneno makali ya Yesu. “ngoa jicho lako” au “ukate mkono wako na kuutupa mbali”. Yesu alitumia lugha hii kali ili aweze kuweka mbele ya wafuasi lengo moja katika maisha ambalo ni maisha safi ya sadaka- hii ikiwa ni muunganiko wa matakwa yetu na Mungu. Kama Daktari anavyoweza kuondoa mguu au sehemu ya mwili kwamanufaa ya mwili mzima, nasi pia tunapaswa tuwe tayari kuachana na kile kinachoweza kutufanya tutende dhambi, na ambacho kwa njia yeyote kitatuletea kifo cha roho zetu. Yesu pia anatuonya sisi pia tuwe na jukumu kubwa la kutokuwa kikwazo au kisababishi cha kuwafanya wengine watende dhambi, au kuwaangusha, tusiwe kipingamizi au tusitoe mfano mbaya ambao utawaongoza wengine kwenye dhambi.

Pili, Yesu anatufundisha kwamba kuwa safi ni pamoja nakuwa tayari kukabili kila hali katika maisha katika hali ambayo inatimiza sheria ya Mungu, si tu katika matendo ya njee bali na ya ndani pia. Yesu anasema tamaa mbaya hutoka moyoni. Ndio maana dhambi yakukosa uaminifu ni lazima itibiwe kwanza kutoka ndani ya moyo, sehemu ambayo si ya hisia tuu, bali utashi, maamuzi, mawazo, na malengo pia. Ni lazima tutambue lengo la Amri za Mungu na tuamue kutoka moyoni kumfuata Mungu.

Sala: Bwana, nisamehe kwa sababu ya dhambi zangu, ninaomba huruma yako na msamaha. Nisaidie niweze kuacha yote yanayo nipeleka kwenye dhambi na kukabidhi mawazo na matendo yangu kwako kila siku. Yesu, nakuamini wewe. Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni