Alhamisi, Agosti 04, 2016
Alhamisi, Agosti 4, 2016,
Juma la 18 la Mwaka
Kumbukumbu ya Mt. Yohane Maria Vianney, Padre.
Yer 31:31-34;
Zab 50: 12-15, 18-19;
Mt 16:13-23
MUNGU ANAANDIKA KATIKA MIOYO YETU!
Leo, Yeremia anaruhusiwa kutoa ujumbe wa matumaini. Taswira kutoka somo la kwanza ya Mungu kuandika sheria zake mioyoni mwetu, inafariji sana na imefanyika ili kututia nguvu na ujasiri. Mungu anamvuvia Yeremia awaambie watu kwamba Mungu anatambua madhaifu yetu na jitihada zetu na pia kutambua kwa nguvu zetu wenyewe hatuwezi kuzishika na kutimiza sheria zake. Taswira ya kuandika inaweza kutufanya tutambue kikwazo kimoja. Kwa kweli, tunaweza kukiri wote kwamba, pengine tusingiweza kila mara kuwa vyombo imara kila wakati vya Mungu kuandikia. Tusingeweza pengine kushirikiana na Mungu kila wakati pale ambapo angependa kumalizia “kazi yake ya kuandika”. Mungu hana chochote kibaya kuhusu uwezo wake wa kuandika sheria zake mioyoni mwetu, lakini sisi tunampinga. Wakati mwingine anachokataka kuandika Mungu mioyoni mwetu hakikai katika undani wa mioyo yetu.
Kwa hiyo tunaalikwa kuweka taswira au picha hii, kuona kwamba Mungu kwa huruma yake na uvumilivu wake kwetu hachoki kututafuta. Anaendela kuandika. Mungu anajua kwamba kuna wakati atabidi aandike tena na kupitia, kufuta na kuweka upya, kufuta kabisa baadhi ya sehemu au kufuta yote na kuandika upya. Kwa hakika, njia mbili za pekee ambazo Mungu anatumia kuandika katika mioyo yetu ni kupitia Maandiko Matakatifu, ujumbe wake tunao usikia kwa njia ya Maandiko Matakatifu naya pili ni Neema ya Mungu inayofanya kazi katika Kanisa kwa njia ya Sakramenti. Tutumie sakramenti kufuta na kuandika tena kwa kushirikiana na neema ya Mungu.
Sala: Bwana, naomba unifanye nishirikiane nawe and niwe chombo chako cha kuandika maneno yako. Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni