Ijumaa. 17 Mei. 2024

Tafakari

Jumamosi, Juni 10, 2017

Jumamosi, Juni 10, 2017.
Juma la 9 la Mwaka

Jumamosi kumbukumbu ya Bikira Maria.

Tob 12:1, 5-15, 20;
Tob 13:2, 6-8;
Mk 12: 38-44.


MKARIMU KAMA MJANE MASKINI!

Somo la Injili linatoa picha Yesu akiwa na wafuasi wake, akiwa amekaa akiangalia watu wakiwa wanatoa sadaka hekaluni. Wale watu waliopenda kuonekana kuwa watu wa karimu walitoa nyingi sana. Lakini tazama anatokea mjane maskini, ambaye katika hali ya ukimya na unyofu anaweka senti mbili. Yesu mara moja anavutwa na kitendo hichi na anawaambia wafuasi wake. Aliweka senti mbili tu kiasi ambacho kilikuwa ni kidogo sana. Lakini tazama Yesu anamtangaza kwamba ametoa nyingi zaidi kuliko wengine. Yesu anaelezea tofauti juu ya utajiri wa kimwili na utajiri wa kiroho. Utajiri wa kiroho na ukarimu wa kiroho ni muhimu zaidi kuliko utajiri wa kimwili. Mjane huyu alikuwa maskini kimwili lakini alikuwa tajiri kiroho. Wale waliokuwa na kiasi kikubwa cha fedha walionekana kuwa matajiri wa kimwili lakini maskini wa kiroho kuliko mjane huyu.

Katika ulimwengu wa kutafuta mali tunaoishi katika, ni vigumu kuamini. Ni vigumu kugeuza dhamiri na kugeukia utajiri wa kiroho wenye Baraka nyingi. Tunapaswa kuwa kama huyu mjane maskini na kutoa yote tulionayo. Alitaka kuleta tofauti. Alitoa yote aliokuwa nayo.

Kila mtu anapaswa kuangalia ni kwa jinsi ghani hili linaingia katika maisha yake. Tunapaswa kuwa na hali ya ndani ya kuwa na ukarimu na hali ya kuachia. Kuanzia hapa, Bwana atakuonesha ni kwa jinsi ghani ya kutumia mali zetu kwa ajili ya faida ya uzuri wetu na kwa ajili ya wengine pia. Toa ulionayo na jinsi ulivyo kwake, naye ataelekeza moyo wako kadiri ya utukufu wake mkamilifu.

Sala: Bwana, ninaomba unipe moyo wa ukarimu na uondoe moyo wa ubinafsi kama yule mjane. Nisaidie mimi nitafute njia za kujitoa kabisa kwako, bila kushikilia mambo mengine nyuma yangu, na zaidi kutafuta utukufu wa kiroho katika ufalme wako. Yesu, nakuamini wewe. Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni