Alhamisi. 16 Mei. 2024

Tafakari

Ijumaa, Juni 09, 2017

Ijumaa, Juni 9, 2017,
Juma la 9 la Mwaka

Tob 11:5-17;
Zab 145:2, 7-10;
Mk 12: 35-37.


FURAHIA NDANI YA BWANA!

Sisi Wakristo tunafahamu kwamba Yesu ni Masiha, Mwana wa Daudi. “Mwana wa Daudi” jina linalo mwakilisha Yesu huku likitengeneza uti wa mgongo wa Injili. Katika Maamkio ya Bikira Maria alipokea ujumbe huu “Na Bwana Mungu atampa kiti cha Daudi Baba yake, na atatawala nyumba ya Yakobo milele, na Ufalme wake hautakuwa na Mwisho” (Lk 1:32-33). Yule Maskini aliyekuwa mwombaji alimwomba Yesu amponye, akisema “Yesu Mwana wa Daudi, unihurumie mimi” (Mk 10:48). Wakati Yesu alivyokuwa akiingia Yerusalemu walimshangilia wakisema “Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana, hosanna juu mbinguni” (Mk 11:10).

Lakini sio tu Mwana wa Daudi, yeye pia ni Bwana. Analionesha hili yeye mwenyewe kwa kunukuu zaburi ya Daudi 110. Mt. Petro, aliye shahidi wa ufufuko wa Bwana, aliona wazi kwamba Yesu amethibitiswa “Bwana wa Daudi”, kwasababu “ndugu zangu nina waambia kwa ujasiri kwamba Babu yetu Daudi alikufa na akazikwa na kaburi lake lipo hapa hadi leo…lakini Yesu ambaye ni Mungu alifufuka, ambao sisi ni mashahidi wake.” (Mdo 2:29-32).

Leo Yesu anajaribu kuwaelewesha Wayahudi kuhusu Masiha au Kristo. Masiha atakuwa Daudi mpya, akitawala juu ya Ufalme wake, lakini atatawala milele katika ufalme wa milele, kama Malaika Garieli alivyo tangaza kwa Maria (Lk 1:32-33; Is 9:7). Atakuwa Mwana wa Mungu kwa asili, na hivyo atakuwa Mungu mwenyewe, mwenye Umungu sawa na Baba.

“Umati mkubwa walisikia hili kwa shauku na furaha (Mark 12:37). Mafundisho ya Yesu yalileta furaha sana katika mioyo yao. “Je, mimi nina yarufahia maneno ya Yesu?” ni mara nyingi tunayaona maneno ya Yesu kama mzigo, au kuwa kikwazo kwa mambo ambayo tunataka kufanya katika maisha. Furaha katika Bwana ni kitu ambacho kinatufanya kukuwa zaidi kila siku. Tujiruhusu kufurahi katika Bwana na kufurahia uwepo wa maneno yake. Tukiwa “tumeiva vizuri” tutamtafuta yeye zaidi.

Sala: Bwana Yesu, Mwana wa Daudi, ninatamani kufurahia katika wewe. Nisaidie niweze kuacha mambo yote ya ulimwengu yanayo niweka mbali nawe. Nisaidie niweze kukutafuta wewe na neno lako daima. Jaza roho yangu na furaha yako. Yesu, nakuamini wewe. Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni