Alhamisi. 16 Mei. 2024

Tafakari

Jumatatu, Juni 05, 2017

Jumatatu, Juni 5, 2017.
Juma la 9 la Mwaka

Kumbukumbu ya Mt. Bonifasi, Askofu na Shahidi

Tob 1:3, 2:1-8;
zab 111: 1-2,3-6;
Mk 12: 1-12.


MWAMINI BWANA!

Mfano kutoka katika Injili unalekeza katika haki ya Mungu! wale watumwa wabaya waliwaua mtumishi mmoja baada ya mwingine, na hata Bwana wa Shamba alivyo mtuma mwanaye wa pekee, wale wamtumwa wabaya walimua pia wakidhani watauchukua urithi wake. Hili linaelekeza kwa Baba alivyo mtuma Mwanae wa pekee Yesu kuja ulimwenguni. Viongozi wa dini wa kipindi hicho, kwa chuki na wivu walitaka kubaki katika uongozi na mamlaka. Wakatenda kwa ubaya, wakumuua Yesu wakidhani watakuwa wamemuondoa yeye kutokuwa Masiha na Mfalme wa Israeli, na hivyo wao kulinda mamlaka na madaraka yao. Lakini haki ya Mungu daima ina ngara. Mungu huchambua kila kitu na hugawa haki yake na huruma kadiri ya moyo wa kila mtu.

Jinsi Mungu anavyotenda na jinsi mwanadamu anavyofikiri ni vitu viwili tofauti kabisa kiasi ambacho mwanadamu anajiandaa akidhani atashambuliwa. Wema haujajikita katika kutoa mengi tu, bali kutoa hata kidogo kwa wakati. Mungu alimtoa mwanaye kwa wakati kwa ajili yetu. Alitupa yote kwa wakati. Yesu aliongea na kutenda katika hali ambayo watu kwakuona anayosema nakutenda, wakatambua Mungu ni wa namna ghani. Kwa maneno mengine, Yesu hakuongea tuu kuhusu Mungu na kuonyesha muelekeo wa kwenda kwake, bali alionesha uwepo wa Mungu na Mungu akaonekana akiwa kati ya watu wake. Kama sio yeye, Mungu kwetu angekuwa ni kama kitu tuu cha kutumaini nakutafuta. Lakini kwa njia yake Mungu yupo kati yetu (Ekaristi Takatifu). Kabla ya Yesu, hakuna aliyejua sifa za Ufalme wa Mungu ulivyo, yeye ndiye aliyetupa mifano akielezea jinsi Ufalme wa Mungu ulivyo, na akatuambia yeye amekuja kuutangaza, upo kati yetu, na bado utatimilizwa katika maisha ya umilele. Kwahiyo tukiishi vizuri na wengine tunaishi Ufalme wake tukiwa hapa duniani.

Yesu, hakutaka chochote kwa ajili yake binafsi, bali kila kitu alichokuwa nacho na kutenda, alifanya kwa ajili ya wengine. Kila mmoja wetu ni wa Yesu, chombo cha upendo wa Mungu, na chombo chakupokea wema wa Mungu. Leo tujiulize kama tumekuwa wazi kwa wema na upendo huu wa Mungu.

Mara nyingi Mungu wetu mkarimu anaruhusu wakati mwingine tuone mashaka juu ya haki yake. Lakini tunapaswa kumwamini Mungu na kubaki waaminifu na kuweka matumaini yote kwa Mungu. Ukijikuta mara nyingine una katishwa tamaa kwa ukosefu wa haki na magumu, jaribu kugeukia utukufu wa mwisho wa Kristo. Tambua kabisa Mungu ataleta haki kamili. Wakati huo, utafurahia kwamba ulimtumainia na kuamini ahadi yake.

Sala: Bwana, wakati nikiwa chini na kukata tamaa na kushuhudia uonevu na ukosefu wa haki katika maisha yangu, nifanye daima nielekeze macho yangu kwako daima na kupata tumaini. Ninakuomba daima niwe na tumaini na Imani katika wema wako kamili. Yesu, nakuamini wewe. Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni