Jumanne. 30 Aprili. 2024

Tafakari

Jumamosi, Mei 20, 2017

Jumamosi, Mei, 20, 2017.
Juma la 5 la Pasaka

Mdo 16: 1-10;
Zab 100: 1-3,5 (R. 1);
Yn 15: 18-21.


KUKUTANA NA MATESO

Mkristo kwa Sakramenti ya Ubatizo ni mmisionari. Anaitwa kushirikisha Habari Njema kwa kila mtu . katika ubatizo, Mkristo hufufuka kutoka katika hofu ya kifo, na kwenda kwenye utukufu wa uzima wa milele. Sisi sio watu tuliofungwa na dunia bali watu tuliofungwa na Mbinguni. Na hii safari ya kwenda mbinguni sio rahisi, kwasababu thamani na hali ya maisha ya Kikristo ni tofauti na hali ya kawaida ya kufikiri.

Ni rahisi kufikiri kwamba kadiri tunavyokuwa karibu na Yesu ni kadiri hiyo hiyo tutakavyo pendwa na kueleweka na Ulimwengu. Tunadhani kwamba kila mtu atapendezwa na kuvutwa na utakatifu wetu na kuwa watu wazuri kwetu. Lakini sivyo. Tukiangalia maisha ya Yesu, tunatambua kuwa haikuwa hivyo. Alikuwa wazi ni mkamilifu kwa kila kitu. Lakini, walimtenda vibaya na kumsulubisha. Alishikwa na kupigwa na kutukanwa na kuhukumumiwa kifo.

Kama tungekuwa pale, tungeweza kushangazwa sana, na kuchanganyikiwa. Tunaweza kufikiri kwamba Yesu alikosea na hivyo kupoteza matumani kwake. Lakini mpango wake ulikuwa mkamilifu kwa kila njia na mpango wake ulikuwa katikati na kumfanya yeye kuvumilia dhuluma za uongo na kuteswa. Na kwa uhuru kukubali kushutumiwa, aliikomboa dunia.

Ukristo ni dini inayo onewa kuliko zote duniani. Asimilia kumi ya wakristo ulimwenguni wananyanyaswa na kuonewa kwasababu tu ya imani yao. Kunyanyaswa na kuonewa kunaleta hofu na uchungu. Lakini sio kitu ambacho tunapaswa kukikimbia. Hatupaswi kupoteza matumaini yanavyotokea haya. Kwanini? Kwasababu manyanyaso ni ishara wazi tunafuata njia sahihi ya Yesu. Tumeungana na Yesu zaidi katika njia ya kuonewa na kudhulimiwa kuliko hata tunavyofikiri. Ufunguo ni kutambua kwamba Mungu atatumia madhulumu yote kuwa furaha yetu kama tutamruhusu. Na tutamrushu ayatumie kwa kuleta mema kama tutajikabidhi kwake kwa uhuru kabisa. Majibu yetu yanapaswa kuwa “furahi na kushangilia” kwani tumekuwa sahihi katika kufuata njia ya Bwana wetu, Mwana wa Mungu.

Leo tutazame katika hali yeyote ya kuonewa na kudhulumiwa au kukosewa haki tunayo ipata kwasababu ya Imani yetu na kushika Injili. Tuwaombee pia Wakristo wanaodhulumiwa huko Syria, Misri, China, Pakistani, India nk.

Sala: Bwana, nina kabidhi kwako yale yote yanayo niangusha chini. Ninatoa sadaka yote ninayo pokea kwa kuwa mtumishi na mfuasi wako. Ninaomba nisikuige wewe tu katika mateso yako, bali kutii mapenzi yako daima. Yesu, nakuamini wewe. Amina

Maoni


Ingia utoe maoni